Majukumu ya Kitengo cha Ukaguzi wa ndani
1. Kutoa ushauri kwa maafisa masuuli kuhusu namna bora ya kusimamia rasilimali.
2. Kupitia na kutoa taarifa kuhusu namna bora ya kutumia na kuifadhi rasilimali fedha za Halmashauri.
3. Kupitia na kutoa taarifa kuhusu uzingatiwaji wa kanuni na miongozo ya matumizi inayotolewa na mhasibu mkuu wa serikali ili kuwa na matumizi bora a fedha.
4. Kupitia na kutoa taarifa kuhusu ubora wa mifumo ya kompyuta iliyopo katika kusimamia matumizi bora a fedha.
5. Kupitia na kutoa taarifa kuhusu mifumo iliyopo katika Halmashauri inayosimamia mali kama inakidhi mahitaji ya matumizi bora.
6. Kuandaa mpango mkakati wa ukaguzi.
7. Kuratibu shughuli za ukaguzi wa ndani.
8. Kufanya ukaguzi kuhusu thamani halali ya fedha kwa huduma na bidhaa zilizonunuliwa.
Halmashauri ya Wilaya ya Ushetu
Anuani: S. L. P 50 Kahama
Simu: 0759888848
Simu ya kiganjani: 0759888848
Barua pepe: ded@ushetudc.go.tz Tovuti www.ushetudc.go.tz
Hati Miliki ©2017 Halmashauri ya Wilaya ya Ushetu . Haki zote zimehifadhiwa