Halmashauri ya wilaya ya Ushetu ina shule 18 za sekondari katika Kata 16 zenye kidato cha 1-4, miongoni mwa shule hizi shule moja ya Dakama ina wanafunzi wa kidato 5 & 6 katika Tahasusi za PCM na HGL ambao walianza mwezi Julai, mwaka 2015 baada ya shule hii kupata kibali cha kuwa na wanafunzi wa kidato cha tano (5) na sita (6). Shule hizi zote ni za serikali na Halmashauri ya Wilaya ya Ushetu haina shule yeyote ya sekondari inayomilikiwa na mtu binafsi au shirika.
Shule zilizopo zina jumla ya wanafunzi 5,590 ambapo wavulana 3078 na wasichana 2512.
Idadi ya walimu katika shule za sekondari.
uwiano wa mwalimu kwa wanafunzi katika shule za sekondari
S/N
|
Kata
|
S/N
|
Jina la shule
|
Idadi ya wanafunzi
|
Idadi ya walimu
|
Uwiano wa Mwalimu: wanafunzi
|
|
1
|
Mpunze
|
1
|
Mpunze
|
396
|
17
|
1:23
|
|
2
|
Nyamilangano
|
2
|
Kisuke
|
535
|
21
|
1:25
|
|
3
|
Bulungwa
|
3
|
Bulungwa
|
455
|
19
|
1:23
|
|
4
|
Chambo
|
4
|
Chambo
|
282
|
17
|
1:16
|
|
5
|
Chona
|
5
|
Chona
|
339
|
11
|
1:30
|
|
6
|
Ukune
|
6
|
Dakama
|
435
|
22
|
1:20
|
|
|
Ukune
|
7
|
Ukune
|
133
|
13
|
1:10
|
|
7
|
Idahina
|
8
|
Idahina
|
249
|
12
|
1:20
|
|
8
|
Ushetu
|
9
|
Mweli
|
252
|
16
|
1:15
|
|
|
Ushetu
|
10
|
Ushetu
|
230
|
17
|
1:13
|
|
9
|
Ulewe
|
11
|
Ulewe
|
375
|
12
|
1:31
|
|
10
|
Ulowa
|
12
|
Ulowa
|
590
|
16
|
1:36
|
|
11
|
Uyogo
|
13
|
Uyogo
|
261
|
14
|
1:18
|
|
12
|
Kinamapula
|
14
|
Kinamapula
|
356
|
16
|
1:22
|
|
13
|
Igwamanoni
|
15
|
Igwamanoni Sekondari
|
280
|
16
|
1:18
|
|
14
|
Igunda
|
16
|
Igunda
|
142
|
8
|
1:18
|
|
15
|
Nyankende
|
17
|
Nyankende
|
132
|
11
|
1:12
|
|
16
|
Sabasabini
|
18
|
Sabasabini
|
148
|
8
|
1:18
|
|
17
|
Ubagwe
|
|
-
|
|
|
|
|
18
|
Kisuke
|
|
-
|
|
|
|
|
19
|
Mapamba
|
|
-
|
|
|
|
|
20
|
Bukomela
|
|
-
|
|
|
|
|
|
JUMLA
|
5590
|
266
|
1:21
|
Halmashauri ina walimu 266, kama takwimu zinavyoonesha hapo juu, kwa mtizamo wa kawaida walimu waliopo wanaotosheleza mahitaji hususani kwa masomo ya sanaa na lugha. Changamoto kubwa iko upande wa walimu wa sayansi na hisabati ambapo hadi sasa upo upungufu wa walimu 100.
Maendeleo ya Taaluma
Shule za sekondari katika halmashauri ya wilaya ya Ushetu zimekuwa zikifanya vizuri mwaka hadi mwaka, mfano jumla ya wanafunzi 124 waliomaliza kidato cha nne mwaka 2014 walichaguliwa kujiunga na masomo ya kidato cha 5 katika shule mbalimbali za serikali na wanafunzi wengine walijiunga na vyuo mbalimbali katika ngazi za astashahada na stashahada na asilimia ya ufaulu kiwilaya ilikuwa 79.83.
Katika matokeo ya mtihani wa Taifa wa kidato cha nne mwaka 2015, jumla ya wanafunzi 568 wamefaulu mtihani na asilimia ya ufaulu kiwilaya ni 80 ikiwa ni ongezeko la ufaulu wa asilimia 0.17 ukilinganisha na ufaulu wa mwaka 2015.
Jedwali lifuatalo linaonyesha hali ya ufaulu wa mtihani wa kidato cha 4 kwa miaka mitatu
Mwaka Idadi ya watahiniwa
Mwaka
|
Idadi ya watahiniwa
|
daraja |
% ya ufaulu |
||||||||||
I
|
II
|
III
|
IV
|
0
|
|||||||||
wav
|
was
|
wav
|
was
|
wav
|
was
|
wav
|
was
|
wav
|
was
|
wav
|
was
|
||
2014
|
333
|
148
|
6
|
0
|
41
|
4
|
78
|
19
|
131
|
82
|
57
|
35
|
79.83
|
2015
|
445
|
265
|
5
|
0
|
30
|
5
|
67
|
31
|
160
|
117
|
49
|
63
|
80
|
2016
|
409
|
339
|
3
|
0
|
44
|
6
|
77
|
24
|
209
|
171
|
76
|
138
|
71.39
|
Uandikishaji wa wanafunzi wa kidato cha 1 mwaka 2017
Hadi tarehe 2/02/2017 jumla ya wanafunzi 1900 sawa na asilimia 91 ya lengo la wanafunzi 2,080 walikuwa wamesharipoti shule na wanaendelea na masomo, na wanafunzi 176 sawa na asilimia 8 ya hawajaripoti katika shule walizopangiwa na majina yao yamepelekwa kwa watendaji wa kata na vijiji kwa ajili ya kubaini sababu za kutoripoti kwao ikiwa ni pamoja na kuchukuliwa hatua za kisheria kwa wazazi/walezi waliopuuza agizo la serikali la kuwapeleka shule watoto wao.
Hali ya miundombinu katika Shule za Sekondari na upatikanaji wa vitabu.
Miundombinu katika shule za sekondari.
NA
|
AINA YA MIUNDOMBINU
|
MAHITAJI
|
VILIVYOPO
|
PUNGUFU/ZIADA
|
1
|
Jengo la Utawala
|
18
|
14
|
4
|
2
|
Vyumba vya madarasa
|
146
|
135
|
22
|
3
|
Nyumba za walimu
|
266
|
55
|
211
|
4
|
Vyumba vya maabara
|
54
|
45
|
9
|
5
|
Viti
|
5842
|
4,594
|
1248
|
6
|
Meza
|
5842
|
4,803
|
1039
|
6
|
Vyoo ( matundu)
|
262
|
242
|
20
|
Halmashauri inaendelea kuboresha miundombinu ya shule, ikiwemo vyumba vya madarasa, na nyumba za walimu.
Katika kuendelea kutatua changamoto ya upungufu wa nyumba za walimu Halmashauri imepokea Tsh. 496,291,888 kutoka Serikali Kuu ambazo ni kwa ajili ya ujenzi wa vyumba 2 madarasa, nyumba ya walimu (6 in 1) na vyoo matundu 8 katika shule za sekondari za Idahina na Ulewe. Fedha hizi ziko kwenye Mpango wa Maendeleo katika Elimu ya Sekondari (MMES II)
Halmashauri ya wilaya ya Ushetu inaipongeza serikali kwa kutimiza azima yake ya kutoa elimu ya msingi bila malipo yani elimu ya chekechekea hadi kidato cha nne kuanzia mwezi Disemba 2015.
Hadi kufikia sasa Halmashauri imeshapokea jumla ya Tsh. 154,110,000 kwa ajili ya elimu bila malipo ambazo zilitumwa moja kwa moja katika akaunti za shule, fedha hizi zinatumika kwa ajili ya chakula cha wanafunzi wa bweni, fidia ya ada ya bweni, fidia ya ada kwa wanafunzi wa kutwa, ununuzi wa vifaa vya kujifunzia na kufundishia ambavyo ni pamoja na ununuzi wa tufe, kemikali na vivunge vya sayansi pamoja na shughuli za uendeshaji wa shule kwa ujumla.
Mafanikio
Changamoto.
Mikakati.
Halmashauri ya Wilaya ya Ushetu
Anuani: S. L. P 50 Kahama
Simu: 0759888848
Simu ya kiganjani: 0759888848
Barua pepe: ded@ushetudc.go.tz Tovuti www.ushetudc.go.tz
Hati Miliki ©2017 Halmashauri ya Wilaya ya Ushetu . Haki zote zimehifadhiwa