Hali ya Mawasiliano katika Halmashauri
Mawasiliano ya Intaneti yanapatikana kwa njia ya WAN (Wide Area Network) na WIFE (Wireless Fidelity) ambap Teknolojia inayotumika ni VSAT (A very small aperture terminal)
Mifumo ya Kompyuta iliyopo:
Mifumo Mingine inayotumika Katika ngazi ya Halmashauri ni Mfumo wa taarifa za UKIMWI (TOMSHA), Mfumo wa taarifa za TASAF, Mfumo wa taarifa za Mfuko wa Afya ya jamii (CHF)
Majukumu ya Kitengo cha TEHAMA:
1. Kusimamia utekelezaji wa sera ya Serikali Mtandao na Teknolojia ya Habari na Mawasiliano katika Halmashauri.
2. Kuhakikisha vifaa vya kompyuta na mtandao wa mawasiliano vinakuwa katika hali nzuri.
3. Kusaidia na kutoa huduma za manunuzi ya vifaa vya kompyuta na Mtandao wa Mawasiliano katika Halmashauri.
4. Kuanzisha na kusimamia matumizi ya mawasiliano ya baruapepe, mtandao wa ndani na nje ya Halmashauri
6. Kuratibu na kusimamia uanzishwaji wa mifumo ya kompyuta na benki za takwimu katika Halmashauri
7. Kuratibu na kusimamia uendelezaji wa watumishi katika matumizi ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA).
8. Kufanya tafiti zinazohusiana na utumiaji wa teknolojia ya mawasiliano kama chombo cha kuimarisha utendaji, utoaji wa taarifa muhimu na huduma kwa wananchi na wadau wote.
9. Kutoa huduma za kitaalamu katika matumizi ya Teknolojia ya Habari kwa Halmashauri.
10. Kutekeleza sera ya Serikali ya mtandao (e-government)
11. Kuandaa na kuratibu utekelezwaji wa mfumo wa mawasiliano kwa kutumia kompyuta (MIS).
10. Kuratibu na kutoa ushauri wa kitaalamu katika maununuzi ya vifaa vya teknolojia ya habari.
11. Kuhakikisha kuwa vifaa vya tekolojia ya habari vinatunzwa kwa matumizi endelevu.
12. Kuanzisha na kuratibu matumizi ya mfumo wa mawasiliano ya barua pepe ndani ya Halmashauri na mifumo ya LAN na WAN.
13. Kufanya utafiti na kushauri maeneo ya kutumia Teknolojia ya Habari ili kuboresha ufanisi.
14. Kutoa huduma za kitaalamu kuhusu habari, Elimu na Mawasiliano kati ya Halmashauri na Umma pamoja na vyombo vya habari.
15. Kuandaa na kusambaza vipeperushi, majarida kwa lengo la kuelimisha umma sera na maboresho mbalimbali yanaotekelezwa na Halmashauri.
16. Kuratibu mikutano na waandishi wa habari.
17. Kutoa habari kuhusu sera, programu na shughuli mbalimbali za Halmashauri.
18. Kushauri Idara, vitengo na idara zinazojitegemea katika kuandaa taarifa mbalimbali kwa ajili ya umma.
Halmashauri ya Wilaya ya Ushetu
Anuani: S. L. P 50 Kahama
Simu: 0759888848
Simu ya kiganjani: 0759888848
Barua pepe: ded@ushetudc.go.tz Tovuti www.ushetudc.go.tz
Hati Miliki ©2017 Halmashauri ya Wilaya ya Ushetu . Haki zote zimehifadhiwa