Idara ya Maji
Katika eneo la Ushetu, asilimia 47 ya wakazi wa vijijini wanapata maji safi na salama, Vyanzo vikuu vya huduma ya maji katika eneo la Halmashauri ni visima vifupi, virefu, matanki ya kuvuna maji ya mvua, visima vya asili na malambo.
• Halmashauri imefanikiwa kuanzisha na kukamilisha miradi mikubwa ya usambazaji wa maji katika kata za Bulungwa na Nyamilangano. Miradi hii iko kwenye hali nzuri na wakazi wa maeneo hayo wananufaika na mradi kwa kutumia maji safi na salama. Halmashauri pia iko kwenye hatua za umaliziaji wa miradi mikubwa ya maji ya chambo na Kayenze.
• Halmashauri imefanikiwa kuchimba visima vifupi ishirini na nne (24) katika maeneo ya kata ya Chona, Mapamba, Ulowa, Ushetu, Igwamanoni, Igunda, Kisuke, Nyankende, Ulewe, Sabasabini, Bukomela, Bulungwa na Idahina.
Halmashauri ya Wilaya ya Ushetu
Anuani: S. L. P 50 Kahama
Simu: 0759888848
Simu ya kiganjani: 0759888848
Barua pepe: ded@ushetudc.go.tz Tovuti www.ushetudc.go.tz
Hati Miliki ©2017 Halmashauri ya Wilaya ya Ushetu . Haki zote zimehifadhiwa