Asilimia 85 ya wakazi wa Halmashauri ya Ushetu wanategemea kilimo. Eneo linalofaa kwa shughuli za kilimo na ufugaji ni kilomita za mraba 395,011. Mazao makuu ya chakula yanayolimwa ni Mahindi, Mpunga, Viazi vitamu, Muhogo, Mtama,na jamii ya Mikunde. Mazao ya biashara ni Pamba, Tumbaku, Karanga na Alizeti.
Jina: Anna Ngongi
Cheo: Mkuu wa Idara ya Kilimo na Ushirika
Mawasiliano:+255754442459
SHUGHULI ZINAZOFANYWA NA IDARA:
• Kuelimisha wakulima mbinu bora za kilimo cha mazao ya chakula na biashara. Elimu itolewayo ni kanuni za kilimo bora, matumizi sahihi ya zana bora katika kuboresha kilimo kwa lengo la kuongeza uzalishaji, matumizi sahihi ya mbolea na viuatilifu, hifadhi bora ya chakula.
• Idara inaratibu na kufuatilia upatikanaji na usambazaji wa pembejeo za kilimo kwa kushirikiana na wadau mbalimbali kama ; makampuni ya mbegu na viuatilifu, bodi za mazao, mawakala na wasambazaji.
• Kwa kushirikiana na vituo vya utafiti vya Ukiriguru na Naliendele na makampuni ya mbegu ya ASA, IFFA SEED, Meru –agro-tours & consultants Co.ltd, idara inaendesha mashamba ya majaribio ya uzalishaji wa mazao ya pamba na mbegu bora ya karanga na shamba darasa katika zao la mahindi na pamba.
• Kutoa taarifa za takwimu ya kilimo kitaifa kwa mtandao uliounganishwa ujulikanao kama ‘Agricultural Routine Data System’ (ARDS).
• Kuanzisha, kusimamia na kuendesha vituo vya mafunzo ya wakulima na wafugaji vya kata (Ward Resource Centers)
• Kutoa taarifa za maendeleo ya kilimo na hali ya chakula kila wakati ngazi ya Wilaya,Mkoa na Kitaifa
• Kushirikiana na wadau mbalimbali toka sekta binafsi kama HALVETAS na Red Cross.
• Kuhamasisha uanzishwaji wa vyama vya ushirika, kusimamamia uendeshaji wa vyama vya ushirika, kukagua na kutoa taarifa katika vyama, kusimamia mikutano mikuu ya vyama na kusaidia kutatua migogoro ya vyama kwa kuzingatia kanuni na sheria ya vyama vya ushirika.
Halmashauri ya Wilaya ya Ushetu
Anuani: S. L. P 50 Kahama
Simu: 0759888848
Simu ya kiganjani: 0759888848
Barua pepe: ded@ushetudc.go.tz Tovuti www.ushetudc.go.tz
Hati Miliki ©2017 Halmashauri ya Wilaya ya Ushetu . Haki zote zimehifadhiwa