Idara ya Utawala na Rasilimali Watu ni mhimili wa Uendeshaji wa shughuli za Taasisi hii za kila siku. Katika kutekeleza wajibu wake Idara inamsaidia Mkurugenzi Mtendai (W) wa Halmashauri. Aidha, Idara hii ina jukumu la kuhakikisha kuwa halmashauri ina nyenzo za kutosha za kufanyia kazi, nyenzo hizo ni pamoja na rasilimali watu, fedha, majengo, usafiri, samani, n.k. Idara ya Utawala na Rasilimali Watu pia inao wajibu wa kuwezesha Idara zingine “Line Departments” kutenda kazi zake. Pia ina jukumu la kusimamia utendaji kazi katika Halmashauri kwa kuhakikisha kuwa malengo makuu ya Halmashauri yanafikiwa.
Idara ya Utawala na Raasilimali watu imegawanyhika katika sehemu kuuu mbili:-
MAJUKUMU YA IDARA YA UTAWALA
1. Kuhakikisha watumishi wanafuata Sheria na Kanuni za Utumishi wa Umma;
2. Kutafsiri Sheria na Kanuni za Utendaji kazi kwa watumishi katika eneo la kazi;
3. Kuhakikisha Halmashuri ina vitendea kazi vya kutosha;
4. Kusimamia utendaji wa Masjijala za Halmashuri;
5. Kushughulikia masuala ya Itifaki;
6. Kusimamia Usafiri, Ulinzi na Usalama wa Jengo;
7. Kusimamia matengenenzo ya vitendea kazi vya Halmashuri, Majengo na bustani;
8. Kusimamia ustawi wa wafanyakazi ikiwa ni pamoja na Afya, Usalama, Michezo na Utamaduni;
9. Kusimamia Maadili ya Utumishi wa Umma pamoja na kutoa elimu ya kuzuia na kupambana na Rushwa;
10. Kusimamia masuala Mtambuka kama Jinsia, Ukimwi (HIV/AIDS) na kuwa mwakilishii wa masuala Mtambuka Halmashurini;
11. Kuratibu masuala ya Sekta binafsi katika Halmashuri;
12. Kuratibu Utekelezaji wa Mikakati ya Kuboresha Utendaji Halmashurini;
13. Kushauri juu ya mbinu za kuongeza Ufanisi Halmashurini;
14. Kuratibu Utekelezaji wa Mkataba wa Huduma kwa Mteja;
15. Kuratibu ajira, kuthibitisha kazini, kupandisha vyeo na uhamisho wa watumishi;
16. Kuratibu na kuandaa Mpango wa Mafunzo wa watumishi wa Halmashuri;
17. Kuandaa Mafunzo ya awali ya watumishi;
18. Kuandaa Mpango wa Rasilimali Watu wa Halmashuri na mahitaji ya Wataalamu wa Halmashuri;
19. Usimamizi na uendesheaji wa masuala ya Mishahara;
20. Uratibu wa Mkakati wa Upimaji Utendaji Kazi (OPRAS);
21. Kushughulikia masuala ya likizo za wafanyakazi;
22. Kushughulikia stahili mbalimbali za watumishi;
23. Kushughulikia stahili za watumishi wanapostaafu kazi ama kuacha kazi.
Halmashauri ya Wilaya ya Ushetu
Anuani: S. L. P 50 Kahama
Simu: 0759888848
Simu ya kiganjani: 0759888848
Barua pepe: ded@ushetudc.go.tz Tovuti www.ushetudc.go.tz
Hati Miliki ©2017 Halmashauri ya Wilaya ya Ushetu . Haki zote zimehifadhiwa