Elimu ya Awali
kila shule ya msingi inatakiwa kuwa na darasa la elimu ya awali Halmashauri ya Wilaya ya Ushetu inayo madarasa ya awali 102 kulingana na idadi ya shule za msingi zilizopo. Mpaka sasa jumla ya shule 102 zina madarasa ya awali.
Hali ya uandikishaji wa elimu ya awali
Mwaka
|
Idadi ya shule
|
Idadi ya wanafunzi
|
||
Wavulana
|
Wasichana
|
Jumla
|
||
2015
|
100
|
3,643 |
3,718 |
7,361 |
2016
|
100
|
4,666 |
4,865 |
9,531 |
2017
|
100
|
4,230 |
4,554 |
8,784 |
Elimu ya msingi
Halmashauri ya Wilaya ya Ushetu ina jumla ya shule za msingi 102 zenye wanafunzi 65,205 kati yao wavulana ni 32,313 na wasichana 32,892 kama inavyoonekana kwenye jedwali hapo chini-
Idadi ya wanafunzi wa Shule za Msingi kwa kila darasa MWAKA 2017
|
|
|
|
|
6,460 |
6,518 |
12,978 |
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
32,313 |
32,892 |
65,205 |
Uandikishaji wa darasa la kwanza
Zoezi la uandikishaj wa wanafunzi wa darasa la kwanza kwa mwaka 2017 bado linaendelea kwa nchi nzima ambapo litafikia Tamati machi 31, 2017. Hali ya uandikishaji katika wilaya ya Ushetu kwa kipindi cha miaka mitatu mfululizo inafafanuliwa hapa chini : -
Idadi ya wanafunzi walioandikishwa darasa la kwanza 2015-2017
Mwaka
|
Idadi ya shule
|
Idadi ya wanafunzi
|
%
|
|||||
Waliotarajiwa
|
Walioandikishwa
|
|||||||
Wavulana
|
Wasichana
|
Jumla
|
Wavulana
|
Wasichana
|
Jumla
|
|||
2015 |
99 |
5674 |
6469 |
12143 |
5192 |
5349 |
10541 |
86.80 |
2016 |
100 |
10,397 |
9,127 |
19,524 |
10,946 |
10,410 |
21,356 |
111 |
2017 |
100 |
7,074 |
8,213 |
15,287 |
6,460 |
6,518 |
12,978 |
73 |
Hali ya mahudhurio/utoro:
Baada ya Serikali kutoa tangazo la elimu bure kwa Elimu msingi, kasi ya utoro imepungua na kufikia asilimia 14 kwa kipindi cha kuishia Disemba mwaka 2016. Ambapo kwa kiasi kikubwa ni utoro wa rejareja ambao mikakati kabambe ya kudhibiti utoro huo inaendelea kwa kuwashirikisha viongozi wa Kata na Vijiji kuwachukulia hatua wale wote wanaosababisha utoro.
Viwango vya Ufaulu kwa Darasa la Saba
Hali ya ufaulu kwa darasa la Saba imekuwa ikiendelea kuimarika mwaka hadi mwaka baada ya Halmashauri ya Wilaya ya Ushetu kumegwa kutoka kwa iliyokuwa Halmashauri ya Wilaya ya Kahama. Jedwali lifuatalo hapa chini linaonyesha hali halisi ya ufaulu kwa kipindi chote tangu Halmashauri ya Wilaya ya Ushetu ianzishwe kuanzia mwaka 2013 hadi mwaka 2016;-
Hali ya ufaulu kwa darasa la saba
|
Mwaka |
Waliosajiliwa
|
Waliofanya
|
Waliofaulu
|
%
|
||||||
|
Wav
|
Was
|
Jumla
|
Wav
|
Was
|
Jumla
|
Wav
|
Was
|
Jumla
|
||
|
2013
|
4,475
|
4,828
|
9,303
|
4,338
|
4,722
|
9,060
|
2,213
|
1,655
|
3,868
|
42.63
|
|
2014
|
1,962
|
2235
|
4,197
|
1,893
|
2,172
|
4,065
|
1,076
|
840
|
1,916
|
47.17
|
|
2015
|
1,718
|
1,997
|
3,715
|
1,695
|
1,952
|
3647
|
1,118
|
971
|
2,089
|
57.28
|
|
2016
|
1,671
|
1,832
|
3,503
|
1,653
|
1,822
|
3,475
|
1,096
|
997
|
2093
|
60.23
|
Idadi ya Walimu Katika Shule za Msingi 2017
Halmashauri ya Wilaya ya Ushetu ina upungufu wa walimu kwani mahitaji ni walimu 1,774 waliopo ni 1,025 na upungufu ni 749 sawa na asilimia 42. Kuna mkakati wa kuhakikisha walimu waliopo hawaondoki kwa kutoa motisha mbalimbali kama vile kuwajengea nyumba.Hali ya Miundo Mbinu Katika shule na Upatikanaji wa Vitabu
Vyumba vya madarasa
Halmashauri inahitaji vyumba vya madarasa 1,149, vilivyopo ni 757 na upungufu ni vyumba 692,sawa na asilimia 65. Halmashauri inaendelea na zoezi la kuhamasisha wananchi na wadau mbalimbali ili waweze kuchangia ujenzi wa maboma na Halmashauri iweze kuyamalizia, kwa mwaka 2016/17 kuna mpango wa kumalizia vyumba vya madarasa 17.
Nyumba za walimu
Mahitaji ya nyumba za walimu katika Halmashauri ya Wilaya ya Ushetu ni 1,450 na zilizopo ni nyumba 196, hivyo upungufu ni 1,254. Halmashauri inaendelea na zoezi la kuhamasisha wananchi na wadau mbalimbali ili waweze kuchangia ujenzi wa maboma na Halmashauri iweze kuyamalizia.
(c) Matundu ya Vyoo
Matundu ya vyoo ni changamoto kubwa zaidi inayoikabili Halmashauri ya Wilaya ya Ushetu kwani mahitaji ni matundu 2,940, yaliyopo ni matundu 599 na upungufu ni 2,341 sawa na asilimia 80. Halmashauri inaendelea na zoezi la kuhamasisha wananchi na wadau mbalimbali ili waweze kuchangia ujenzi wa mashimo ya vyoo na Halmashauri iweze kuyamalizia. Katika mpango wa kuboresha mazingira mradi wa “School Wash” umewezesha kuchimbwa matundu ya vyoo vya kisasa 170 vyenye sehemu za haja ndogo kwa wavulana na kwa wasichana vyumba vya kubadilishia usafi wao na vyombo vya maji ya kunawa na vya kutupa taka ngumu na mpaka hivi sasa vyoo hivyo vinatumika.
Hali ya Kutojua K.K.K
Hali ya uelewa wa KKK kwa wanafunzi imekuwa ni changamoto kubwa katika shule zetu za msingi. Walimu wanaendelea kujituma kuhakikisha kwamba wanafunzi wote wanajua KKK baada ya mikakati ya uimarishaji wa ufundishaji kuwekwa katika kikao cha kazi katika shule ya msingi Mseki mwezi Julai, 2016. Matokeo ya kikao hicho yalizaa matunda kwani hadi kufikia mwishoni mwa mwaka wa 2016 wanafunzi 504 kati ya 839 waliokuwa hawamudu vizuri stadi za KKK waliimarika na 335 wanendelea vizuri. Kupitia mradi wa uboreshaji wa elimu wa Equip-Tanzania, ambao unakazia ufahamu wa KKK kwa wanafunzi na unaimarisha mbinu za kufundishia na kujifunzia kwa walimu kwa kuwapa semina za kielimu hususani walimu wa darasa la I na II. Ni matumaini yetu kuwa hadi tatizo la KKK kwa wanafunzi litakwisha kabisa.
Aidha, Serikali imeboresha mtaala wa DRS la I na II kwa kupunguza masomo hadi kufikia 5 ambapo masomo 3 ni Kusoma, Kuandika na Kuhesabu masomo 2 ni Michezo na Dini. Hii inawapa fursa walimu kuweka nguvu katika ufundishaji wa KKK badala ya kumfundisha mtoto masomo mengi.
Elimu ya watu Wazima
Katika kuhakikisha adui ujinga anapigwa vita, H/W ina vituo 2 vya MUKEJA vilivyopo katika Kata za Chambo na Ulowa, lengo kuu ikiwa ni kuwawezesha wananchi kielimu na kiuchumi. Vituo hivi vimepewa cherehani na vifaa vya useremala kwa udhamini wa taasisi ya ‘One Person Project’ kutoka Canada ambao ni marafiki wa Halmashauri, hivyo wanafanya mafunzo ya uzalishaji kwa ushonaji na utengenezaji wa samani mbalimbali.
Aidha, zoezi la kusoma, kuandika na kuhesabu kwa watu wazima ni changamoto kubwa kwa Halmashauri ya Wilaya ya Ushetu, kwani kwa sensa ya Elimu ya Watu Wazima ya mwaka 2016, jumla ya watu wazima ni 150,632, kati yao wanaume ni 73,367 na wanawake ni 77,265. Wasiojua KKK ni wanaume 20,338 na wanawake 27,065 jumla yao ni 47,403 sawa na asilimia 31 ya watu wazima. Ili kupunguza tatizo la KKK kwa watu wazima, Halmashauri inaendelea kuhamasisha kila shule iwe na kituo cha Elimu ya Watu Wazima, kwa sera ya Serikali kwa mwaka 2016/17 “Elimu ya Watu Wazima” imepewa kipaumbele ili kuwezesha jamii kubwa ya watanzania kufuta kama siyo kupunguza ujinga wa kutojua KKK.
Ili kupunguza kiwango cha watu wasiojua KKK Iadara ya Elimu Msingi imeendesha sense ya kuwabaini watoto ambao walistahili kuwa shuleni lakini kutokana na sababu mbalimbali wameshindwa kuwa shuleni, na hivyo kuanzisha vituo kumi vya MEMKWA vyenye jumla ya wanafunzi 509 kwa ajili ya kuwafundisha KKK na baadae kuwaingiza kwenye mfumo rasmi.
Hali ya Huduma za Utamadui na Michezo katika Halmashauri
Katika Halmashauri ya Wilaya ya Ushetu, suala la michezo limezingatiwa kwa kutenga maeneo 10 ya michezo katika kata za Ushetu yenye viwanja 2, Ulowa viwanja 3, Kisuke viwanja 2 na Bulungwa viwanja 3. Aidha shule zote za msingi na Sekondari zina viwanja vya michezo ya mpira wa miguu na pete.
Halmashauri imeweza kusimamia michezo ya UMITASHUMTA kwa mwaka 2015/2016 katika ngazi ya kata, wilaya, mkoa na Taifa kwa michezo ya mpira wa miguu, pete, wavu na mikono, aidha Halmashauri imekuwa ikishiriki katika michezo ya shirikisho la michezo ya serikali za mitaa (SHIMISEMITA).
Changamoto na Mikakati katika Sekta ya Elimu ya Msingi
Changamoto
Pamoja na uandikishaji kuwa mkubwa, bado idadi ya wanafunzi wanaofikia kumaliza elimu ya msingi inakuwa ndogo na hali hii inachangiwa na sababu zifuatazo; -
i. Mwamko duni wa elimu miongoni mwa wanajamii ambapo baadhi ya wazazi husababisha watoto wasiendelee na masomo. Mfano, Wazazi kuwashawishi watoto wao kufanya vibaya katika mitihani yao ya mwisho ili wasifaulu.
ii. Mila na desturi za jamii zilizopitwa na wakati ambapo baadhi ya wanajamii hawaoni umuhimu wa kuwaendeleza watoto wao hususani wa kike na kupelekea kuwepo na ndoa za utotoni.
iii. Baadhi ya familia kuwatumia watoto katika kazi ya kuchunga mifugo na kilimo na tabia ya wafugaji ya kuhamahama kwa ajili ya kutafuta malisho ya mifugo pamoja na kilimo.
iv. Ajira za watoto katika maeneo ya migodi ya wachimbaji wadogo wadogo pia huchangia ongezeko la mdondoko wa wanafunzi.
v. Mazingira magumu kama vile, baadhi ya maeneo kuwa na miundombinu mibovu, upungufu wa nyumba za walimu katika baadhi ya shule, uhaba wa huduma za afya, maji safi na ubovu wa barabara katika maeneo ya vijijini, hali hii hupelekea kushusha ari ya walimu katika kutimiza wajibu wao.
Mikakati ya kuboresha elimu
(i) Kutoa elimu kwa jamii kuhusu umuhimu wa elimu kwa watoto wao katika karne hii ya sayansi na teknolojia.
(ii) Kuelimisha jamii hususani katika kuwaendeleza watoto wa kike na kupunguza ndoa za utotoni zinazosababisha vifo na kuongezeka kwa watoto wa mitaani.
(iii) Kuielimisha jamii hasa ya wafugaji kuwa na kiwango cha mifugo wanayoweza kuimudu kuitunza na kutumia mapato yatokanayo na mifugo katika kuwaendeleza watoto kielimu na pia kuongeza uchumi wa familia na taifa kwa ujumla.
(iv) Kukemea ajira ya watoto wadogo na kuwachukulia hatua za kisheria wale wote wanaoajiri watoto.
(v) Halmashauri kuendelea kuboresha miundombinu kwa kushirikiana na wadau mbalimbali wa maendeleo.
(vi) Kuihamasisha jamii kuwa na idadi ya watoto wanaoweza kuwahudumia kikamilifu, yaani “Kutumia uzazi wa mpango na kupunguza ndoa za mitara”
Halmashauri ya Wilaya ya Ushetu
Anuani: S. L. P 50 Kahama
Simu: 0759888848
Simu ya kiganjani: 0759888848
Barua pepe: ded@ushetudc.go.tz Tovuti www.ushetudc.go.tz
Hati Miliki ©2017 Halmashauri ya Wilaya ya Ushetu . Haki zote zimehifadhiwa