27 Novemba, 2025.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Ushetu, Bi. Hadija Kabojela, akiambatana na wataalamu kutoka Idara ya Elimu msingi na Awali, pamoja na wataalamu kutoka Idara ya Ujenzi na Miundombinu, wametembelea miradi ya maendeleo kwenye shule za Msingi
Kalunde (shule shikizi ya Manungu), Kidanha na Ibelansua.
Katika miradi hiyo, Mkurugenzi Kabojela amesisitiza umuhimu wa kukamilisha miradi mapema na kwa kuzingitia bajeti, huku pia akisisitiza kuzingatia ubora wa miradi yote.
'Nashukru naona miradi inakwenda vizuri na usimamizi wenu, ikiwemo taarifa za miradi mnaandaa vizuri, nawasisitiza kuzingatia muda, miradi iishe kwa wakati na iwe yenye ubora unaotakiwa' alisema Kabojela.
Halmashauri ya Wilaya ya Ushetu
Anuani: S. L. P 50 Kahama
Simu: 0767639345
Simu ya kiganjani: 0767639345
Barua pepe: ded@ushetudc.go.tz Tovuti www.ushetudc.go.tz
Hati Miliki ©2017 Halmashauri ya Wilaya ya Ushetu . Haki zote zimehifadhiwa