• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua pepe |
    • Malalamiko |
Ushetu District Council
Ushetu District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Ushetu

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
      • Maadili ya msingi
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya msingi
    • Strategic Plan
  • Utawala
    • Idara
      • Elimu Sekondari
      • Elimu Msingi
      • Biashara na Fedha
      • Kilimo na Ushirika
      • Ujenzi
      • Maji
      • Afya
      • Usafi na Mazingira
      • Takwimu,Mipango na Uchumi
      • Maendeleo ya Jamii na Ustawi wa Jamii
      • Mifugo na Uvuvi
      • Land and Livestocks
    • Vitengo
      • Sheria
      • Manunuzi
      • Teknoloji Habari na Mawasiliano
      • Uchaguzi
      • Ufugaji Nyuki
      • Ukaguzi wa ndani
    • Muundo wa halmashauri
  • Fursa za uwekezaji
  • Huduma
    • Bima ya Afya
    • Mitambo ya kutengenezea Barabara
    • Loan Services
    • Huduma za Afya
    • Education Services
    • Water Services
    • Huduma za Kilimo
    • Livestock Keeping Services
    • Huduma za Uvuvi
    • Human Resources Services
    • Huduma za Leseni za Biashara
    • Land Services
    • Forest Services
  • Madiwani
  • Miradi
    • Uwekezaji
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Taarifa
    • Vifungu vya Sheria
    • Fomu za maombi
    • Zabuni
    • Miongozo
    • Hotuba
  • Kituo cha Habari
    • Hotuba
    • Uhifadhi wa picha
    • Video
    • Habari
    • Matukio

Waheshimiwa Madiwani wa Halmashauri ya Ushetu, wapatiwa mafunzo juu ya namna bora ya kuendesha na kusimamia Mamlaka za Serikali za Mitaa.

Ilipo tumwa: February 5th, 2026

04 Februari, 2026.

USHETU DC.


MAFUNZO hayo yaliyofanyika kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Hospitali ya Wilaya ya Halmashauri ya Ushetu, kwa muda wa siku 3, kuanzia tarehe 2-4 Feb, 2026, yalihudhuriwa na madiwani wote wa Halmashauri ya Ushetu pamoja na wakuu wa Divisheni na Vitengo, yalilenga kuwajengea uwezo kuhusu namna bora ya kuendesha na kusimamia Mamlaka za Serikali za Mitaa.


Wakufunzi kutoka Taasisi ya Mafunzo ya Serikali za Mitaa, Hombolo Dodoma,

Dr. Benedict Sulley, Anorld Kabaitiraki na Bi. Nishafa Ndabakubije, wakiwasilisha mada mbalimbali kwenye mafunzo hayo, ikiwemo Uongozi na Utawala bora, ambapo walielekeza na kufundisha juu ya mambo muhimu ya kuzingatia ili kutimiza adhima ya Utawala na uongozi bora kwenye taasisi.


Katika hatua nyingie, Mada za Sheria za Uendeshaji wa Shughuli za Serikali za Mitaa, Muundo, Majukumu na madaraka ya serikali za mitaa na Uendeshaji wa Vikao na matukio katika Mamlaka za Serikali za Mitaa, ziliwashirishwa kwa ufasaha na wajumbe walipata muda wa kuuliza maswali na kufanya mijadala.


Kwa upande wa mwingine, Mada zinazohusu Mipango, Bajeti na Usimamizi wa miradi ya maendeleo, Usimamizi na udhibiti wa fedha katika Mamlaka za Serikali za Mitaa pamoja na Usimamizi wa Watumishi  na Usimamizi wa Ardhi katika mamlaka ya Serikali za Mitaa, pia ziliwasilishwa.


Mawasilisho mengine yalihusu Wajibu, Majukumu, Haki na Stahiki za Diwani na pia Maadili ya Madiwani, zilifundishwa katka mafunzo hayo.


Wakizungumza wakati wa kuhitimisha mafunzo hayo, Madiwani wa Halmashauri ya ushetu, Wameipongeza Serikali ya mama Samia, kwa kuendelea kuleta fedha nyingi za miradi ya maendeleo kwenye Halmashauri ya Ushetu, na kwa mafunzo waliyoyapata, wameahidi kuongeza ufanisi katika kusimamia na kutekeleza miradi yote ya maendeleo kwenye kata zao.


Na kwa upande mwingine, Madiwani hao, wamemshukru na kumpongeza Mkurugenzi wa Halmashauri ya Ushetu,  Bi. Hadija Kabojela kwa kuwaandalia mafunzo hayo muhimu.


Halmashauri ya Ushetu, inajumla ya Madiwani 27, 20 wakiwa wa kuchaguliwa na 7 ni madiwani wa viti maalumu, huku ikiwa na jumla ya kata 20, vijiji 112 na jumla ya vitongoji 554.

Matangazo

  • Matokeo ya usajili wa Madereva. October 03, 2024
  • Tangazo la kuitwa kwenye Usaili August 22, 2022
  • Tangazo la kuitwa kwenye Usaili August 22, 2022
  • Tangazo la kuitwa kwenye Usaili August 22, 2022
  • Angalia yote

Habari mpya

  • Waheshimiwa Madiwani wa Halmashauri ya Ushetu, wapatiwa mafunzo juu ya namna bora ya kuendesha na kusimamia Mamlaka za Serikali za Mitaa.

    February 05, 2026
  • Kamati ya Fedha, Uongozi na Mipango (FUM), yafanya ziara ya kukagua miradi ya Maendeleo.

    January 28, 2026
  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI

    January 30, 2026
  • Tangazo la Nafasi za Kazi

    January 14, 2026
  • Angalia yote

Video

Kilimo cha Korosho katika Halmashauri ya Wilaya ya Ushetu
Video

Viunganishi vya haraka

  • Kanuni za Utumishi wa Umma
  • Ufafanuzi wa Serikali juu ya Kukosekana kwa Mawasiliano ya simu katika Halmashauri
  • Facebook
  • Ramani ya Halmashauri

Viunganishi Mfanano

  • Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma
  • Ofisi ya Rais-TAMISEMI
  • Baraza la Mitihani
  • Wizara ya Fedha
  • Wakala wa Serikali Mtandao
  • Ajira serikalini

World visitors tracker

world map hits counter

Idadi ya Waliotembelea

free HitCounter

Ramani ya Halmashauri

Wasiliana nasi

    Halmashauri ya Wilaya ya Ushetu

    Anuani: S. L. P 50 Kahama

    Simu: 0767639345

    Simu ya kiganjani: 0767639345

    Barua pepe: ded@ushetudc.go.tz Tovuti www.ushetudc.go.tz

Mawasiliano mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Hati Miliki ©2017 Halmashauri ya Wilaya ya Ushetu . Haki zote zimehifadhiwa