Januari 27, 2026.
Kamati ya Fedha, Uongozi na Mipango ya Halmashauri ya Wilaya ya Ushetu, imefanya ziara ya kukagua miradi ya maendeleo katika Kata mbalimbali za Halmashauri ya Ushetu.
Ziara hiyo iliyofanyika kwa siku mbili, 27_28 Januari, 2026, ilitembelea miradi katika sekta mbalimbali, hasa Elimu, Afya na maji.
Katika ziara hiyo, iliyoongozwa na mweyekiti wa kamati hiyo, ambaye pia ni mweyekiti wa Halmashauri ya Ushetu, Mhe. Gagi Lala Gagi, pamoja na wajumbe kamati hiyo, wakishirikiana na Wataalamu kutoka Divisheni na Vitengo mbalimbali, walifika na kukagua miradi, ikiwa na pamoja na kutoa ushauri wa kitaalamu.
Katika hatua nyingine, wajumbe wa kamati hiyo, walisisitiza umuhimu wa kuzingatia ubora wa miradi, kuzingatia vigezo vya kitaalamu (BOQ) na ukamilishaji wa miradi kwa wakati.
Halmashauri ya Ushetu, inatekeleza miradi katika sekta ya Afya, Wlimu, Kilimo na mifugo, Maji na miradi inayolenga kuwainua wananchi kiuchumi kwa mwaka wa fedha 2025/2026
Halmashauri ya Wilaya ya Ushetu
Anuani: S. L. P 50 Kahama
Simu: 0767639345
Simu ya kiganjani: 0767639345
Barua pepe: ded@ushetudc.go.tz Tovuti www.ushetudc.go.tz
Hati Miliki ©2017 Halmashauri ya Wilaya ya Ushetu . Haki zote zimehifadhiwa