Hayo yamesemwa na Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Ushetu Ndg Athanas Lucas alipokuwa akizungumza na watumishi wa makao makuu katika kikao cha pamoja kilichofanyika makao makuu ya halmashauri hiyo leo tarehe 5 Disemba, 2019.
'Ninawataka kila mmoja afanye kazi kwa kuzingatia kanuni, taratibu na sheria za kiutumishi, ili kuweza kutoa huduma bora na salama kwa wananchi wetu tunaowahudumia' , amesema bwana Athanas.
katika hatua nyingine, afisa Utumishi wa Halmashauri ya Ushetu bi Christina Akiyoo, amewakumbusha watumishi wa Halmashauri hiyo, hasa wale wa makao makuu, kuwahi kazini na kuondoka kulingana na muda wa mwajiri, kwani kinyume na hapo sheria za kiutumishi zitachukua mkondo wake na kuwaadhibu watumishi wote watakaoenda kinyume na taratibu hizo.
Halmashauri ya Wilaya ya Ushetu
Anuani: S. L. P 50 Kahama
Simu: 0759888848
Simu ya kiganjani: 0759888848
Barua pepe: ded@ushetudc.go.tz Tovuti www.ushetudc.go.tz
Hati Miliki ©2017 Halmashauri ya Wilaya ya Ushetu . Haki zote zimehifadhiwa