Maafisa wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) wilayani Kahama, mkoa wa Shinyanga, wameendelea kutoa elimu ya mapambano dhidi ya rushwa katika Halmashauri ya Ushetu, Kata ya Bukomela.
Wananchi wa vikundi vya asilimia 10% wamepatiwa elimu juu ya rushwa kuelekea Uchaguzi Mkuu ujao.
> “Wananchi mnapaswa kuwa wazalendo wa nchi yenu. Tunatambua mchango wenu katika shughuli zenu za biashara ndogo ndogo. Ili muweze kupata kiongozi bora atakayewasaidia kutatua changamoto zenu, mnapaswa kuchagua kiongozi asiyetoa wala kushawishi kwa rushwa.”
Hayo yameelezwa leo na Afisa Msaidizi Bw. Said Karume kwa wanakikundi cha asilimia kumi katika Kata ya Bukomela.
---
UIMARISHAJI WA KLABU ZA MAPAMBANO DHIDI YA RUSHWA
Wanafunzi wa Shule ya Msingi Bukomela wamepatiwa elimu ya mapambano dhidi ya rushwa.
> “Wanafunzi mnapaswa kuwa watii na kuzingatia elimu pamoja na sheria za shule. Mtoto yeyote anayekataa kutekeleza maelekezo ya mzazi mpaka apewe pipi, hiyo ni rushwa na ni tabia mbaya. Tujifunze kuwa na nidhamu tunapokuwa shuleni na nyumbani.”
Kauli hiyo imetolewa na Mchunguzi Msaidizi Bw. Sunday Baregu wakati akitoa elimu ya rushwa kwa wanafunzi wa shule hiyo.
✍
Halmashauri ya Wilaya ya Ushetu
Anuani: S. L. P 50 Kahama
Simu: 0767639345
Simu ya kiganjani: 0767639345
Barua pepe: ded@ushetudc.go.tz Tovuti www.ushetudc.go.tz
Hati Miliki ©2017 Halmashauri ya Wilaya ya Ushetu . Haki zote zimehifadhiwa