18 Agosti, 2025
Kikao hicho cha maelekezo kimefanyika kwenye Ukumbi wa mikutano uliopo kwenye jengo la Hospitali ya Wilaya ya Ushetu na kuhudhuriwa na Maafisa wa Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) Wikaya ya Kahama, bwana Said Karume na Bi. Vicensia, pamoja na wajumbe mbalimbali, wakiwemo Maafisa maendeleo kutoka kila Kata na vijiji.
Akiongea wakati wa kikao hicho, bwana Karume amesisitiza kuwa, fedha za asilimia 10 ya mapato ya ndani ya Halmashauri, kuwa hakuna malipo katika mchakato wa maombi ya mkopo, ila baada ya kupata mkopo kikundi kitahitajika kufanya marejesho ya fedha kamili iliyokopwa kwa mujibu wa mkataba bila riba
Kwa upande wake Bi. Vicensia, amesisitiza kuwa, wanachama wote wa vikundi wanapaswa kusaini mikataba wenyewe, na sio kusainiwa na wawakilishi, na kwamba picha kwenye mikataba ziwe za hivi karibuni zikionyesha uhalisia wao.
Aidha, Kwa namna ya kipekee, maafisa hao kutoka TAKUKURU Wilaya ya Kahama, waliisifia Halmashauri ya Ushetu hasa Idara ya Maendeleo ya Jamii kwa uwazi na ufanisi wa hali ya juu katika kusimamia mikopo hiyo. "Tunawapongeza kwa kufanya kazi kwa weredi, na utendaji kazi wenu hauna shaka hata kidogo na tunatamani hata Halmashauri nyingine wajifunze toka kwenu" amesema bwana Karume.
Kikao hicho kilimalizika kwa kuwakumbusha watumishi kuwa mwaka huu ni wa uchaguzi, hivyo wanapaswa kuhamasisha wananchi kupiga kura na kujiepusha na wanasiasa wanaotoa rushwa.
Halmashauri ya Wilaya ya Ushetu
Anuani: S. L. P 50 Kahama
Simu: 0767639345
Simu ya kiganjani: 0767639345
Barua pepe: ded@ushetudc.go.tz Tovuti www.ushetudc.go.tz
Hati Miliki ©2017 Halmashauri ya Wilaya ya Ushetu . Haki zote zimehifadhiwa