Mkurugenzi wa Halmashauri ya Ushetu mkoani Shinyanga, Hadija Kabojela ametoa motishi ya fedha kiasi cha Sh. 500,000 kwa wakusanyaji sita bora wa mapato waliokusanya zaidi ya Sh.milioni 433.736 kwa mwaka wa fedha 2024/2025.
Kabojela ametoa motisha hiyo wakati akizungumza na wakusanyaji sita kutoka mageti ya makusanyo ya Igunda, Mpunze, Kisuke na Machimbo ya mwabomba hafla iliyofanyika katika Ofisi yake.
Amewataka waendelee kuwa wadilifu na waaminifu na kusisitiza kuwa mapato hayo ndio chachu ya maendeleo ya Halmashauri na wananchi wake hivyo hawapaswi kujihusisha katika udokozi na kusababisha miradi ya maendeleo kutokamilika kwa wakati.
“Niwape hongera sana kwa uchapa kazi Hodari Pamoja na uaminifu mlionao,Endeleeni na moyo huo na msijihusishe na udokozi wa fedha za umma kwani fedha hizi ndizo zinazotekeleza miradi ya maendeleo ya wananchi katika halmashauri yetu,” amesema Kabojela.
Kabojela pia amewataja waliopata motisha ya fedha hiyo kuwa ni pamoja na Mashaka Jifunge wa geti la Igunda amekusanya kiasi cha Sh.milioni 122,776,300, Kashindye Ngele wa geti la Mpunze amekusanya Sh.milioni 102,858,800 na Ambroz John geti la Kisuke amekusanya Sh.milioni 70,152, 700.
“Hakika wamefanya kazi na wanastahili pongezi hii,Yupo Mashaka Jifunge wa geti la Igunda,Kashindye Ngele wa geti la Mpunze,Ambroz John wa geti la kisuke hawa tunawapa motisha ya shilingi laki tano.” Ameongeza Kabojela.
Waliopata motisha ya shilingi laki mbili ni pamoja na Mashaka Tangu wa geti la mpunze amekusanya Sh.milioni 54,443,000, Theonas Banyenda(eneo la machimba ya mwabomba amekusanya Sh.milioni 43,055,000 pamoja na Paul Ngusa geti la Kisuke amekusanya 40,451,000.
“Wanaopata motisha ya shilingi laki mbili ni Mashaka Tungu geti la Mpunze,Theonas Banyenda geti la mahimbo Mwabomba na Paul Ngusa geti la Kisuke,hakika wamefanya vizuri nao pia wanastahili Zawadi.” Amesisitiza.
Kabojela amesema, zawadi hizo zitachochea ari ya utendaji wa kazi katika mageti ya kukusanya mapato na wale ambao hawakupata basi waendelee kukusanya pasi kutojihusisha na vitendo vya odokoaji ili mwaka huu waweze kupata nao motisha kama wenzao.
Kwa upande wao Paul Ngusa na Mashaka Jifunge wamemshukuru mkurugenzi wa halmashauri hiyo kwa kuwapa motisha hizo na wamehaidi kuwa waaminifu ili kuhakikisha mapato hayapotei katika halmashauri hiyo.
“Tunamshukuru sana Mkurugenzi Bi.Kabojela kwa kuweza kutupatia motisha hizi,hakika tutaendelea kuwa waaminifu ili kuhakikisha mapato ya halmashauri hayapotei,” Wamesema.
Halmashauri ya Wilaya ya Ushetu
Anuani: S. L. P 50 Kahama
Simu: 0767639345
Simu ya kiganjani: 0767639345
Barua pepe: ded@ushetudc.go.tz Tovuti www.ushetudc.go.tz
Hati Miliki ©2017 Halmashauri ya Wilaya ya Ushetu . Haki zote zimehifadhiwa