"WALIMU ONGEZENI NIDHAMU KAZINI" DED-KABOJELA
WALIMU wa shule za Msingi katika Halmashauri ya Ushetu wilayani Kahama Mkoani Shinyanga, wametakiwa kuendelea kuwa na nidhamu kazini ili kuongeza ufaulu kwa wanafunzi kutoa 80% kwa darasa la nne na 71% kwa darasa la mpaka kufikia ufaulu 100% kwa mwaka huu 2024.
Agizo hilo limetolewa leo tarehe 07/03, 2024 na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Ushetu Hadija Kabojela, katika kikao cha tathimini ya mitihani ya shule za msingi Ushetu, ambacho kimehudhuriwa na walimu wa shule za Msingi, Maafisa elimu, Madiwani pamoja na Mbunge wa jimbo la ushetu Emmanuel Cherehani.
Kabojela amesema kuwa, ili kuongeza ufaulu kwa mwaka 2024 kila mwalimu anapaswa kuwa na nidhamu ya kazi na kutokuwa na ruhusa za mara kwa mara zisizokuwa na tija pamoja na kuwahizima wazazi kuwapeleka shule watoto wao na kuacha tabia ya kuwapeleka kuchunga ng’ombe ama kulima tumbaku.
Naye, mwenyekiti wa kamati ya Elimu, Afya na Maji, Mhe Doa Limbu amesema kuwa kuna baadhi ya wazazi mpaka sasa hawajapeleka watoto wao shule na kuwataka Wenyeviti wa vijiji na Vitongoji kufatilia watoto wote ambao hawajaenda shule na wamefauli na kuwataka waliripoti shule mapema.
Kwa upande wake Mbunge wa jimbo la Ushetu Emmanuel Cherehani amesema kuwa, ili kuongeza ufaulu kwa wanafunzi, Walimu wanapaswa kuwekewa mazingira mzauri ya kazi kwa kupandishwa madaraja pamoja na kulishughulikia suala la utoro kwa wanafunzi.
Kwa upande mwingine, Afisa taaluma wa Halmashauri ya ushetu Silvanus BONDA, wakati akisoma taarifa ya tathimini ya Mitihani kwa mwaka 2023 amesema, Ufaulu umeongezeka, kwa darasa la nne Kimkoa Halmashauri imeshika nafasi ya kwanza, na darasa la saba nafasi ya nne katika Halmashuri sita za Mkoa wa Shinyanga.
Halmashauri ya Wilaya ya Ushetu
Anuani: S. L. P 50 Kahama
Simu: 0759888848
Simu ya kiganjani: 0759888848
Barua pepe: ded@ushetudc.go.tz Tovuti www.ushetudc.go.tz
Hati Miliki ©2017 Halmashauri ya Wilaya ya Ushetu . Haki zote zimehifadhiwa