WADAU WA MAENDELEO KATIKA HALMASHAURI YA WILAYA YA USHETU WAPEWA MAFUNZO YA MFUMO WA FURSA NA VIKWAZO KWA MAENDELEO (O & OD) ILIYOBORESHWA.
Mafunzo ya Mfumo wa Fursa na Vikwazo kwa Maendeleo (O & OD) Iliyoboreshwa, yametolewa leo tarehe 7 Disemba, 2021, katika Ukumbi wa Mikutano wa Halmashauri ya Ushetu,Mafunzo hayo yalianza muda wa saa 3 asubuhi, ambapo Mbuge wa Jimbo la Ushetu Mh. Emmanuel Cherehani, Madiwani wote wa Halmashauri ya Ushetu, Mkurugenzi wa Halmashauri ya Ushetu ndugu Linno Pius Mwageni, Wakuu wa Idara na Vitengo, Watendaji wa Kata zote za Halmashauri ya Ushetu pamoja na watumishi wengine wa Halmashauri ya Ushetu, kwa pamoja wamepatiwa mafunzo hayo.
Mafunzo hayo yamewezeshwa na wawezeshaji wawili, ndungu Bryan Samuel kutoka OR-TAMISEMI, na Ndugu Rodgers Rugenyomu kutoka Chuo cha Serikali za Mitaa Homboro.
Akizungumza wakati wa ufunguzi wa mafunzo hayo, Mkurugenzi wa Halmashauri ya Ushetu Ndg. Linno Pius Mwageni, aliwataka mashiriki wote kuwa makini na wasikivu ili kuweza kuelewa sawa sawa mafunzo hayo na kuyatumia kwa ufanisi ili kuleta tija kwa jamiii nzima ya Ushetu na Taifa kwa Ujumla.
Katika hatua nyingine, Mwenyekiti wa Halmashauri ya Ushetu Mh. Gagi Lala Gagi, alimshukru Mkrugenzi mtendaji wa Halmashauri kwa kuleta mafunzo hayo, ‘ Ndugu Mkurugenzi, kwa niaba ya sisi Madiwani na wataalamu kutoka Ngazi ya Halmasuari na Kata, naomba nikushukru sana kwa kutuletea Mafunzo haya, kwani yametujengea uwezo mkubwa hasa katika swala zima la kuibua na kutumia Jitihada za wananchi katika kutekeleza na Kukamilisha Miradi katika maeneo yetu. Lakini nikuombe pia katika Bajeti ya mwaka wa Fedha ujao, Ninakuomba uongeze kipengele cha Mafunzo haya, walau tuwe tunafanya hata kwa siku Mbili au tatu ili kujenga uelewa zaidi kuliko hivi tulivyofanya kwa siku moja.’
Mafuzo hayo yalihitimishwa na Mwenyekiti wa Halmashauri Ndugu Gagi Lala Gagi, kwa kuahirisha mafunzo hayo mnamo muda wa saa 10 jioni na kuwatakia washiriki wote utekelezaji mwema kwa yale waliojifunza.
Halmashauri ya Wilaya ya Ushetu
Anuani: S. L. P 50 Kahama
Simu: 0759888848
Simu ya kiganjani: 0759888848
Barua pepe: ded@ushetudc.go.tz Tovuti www.ushetudc.go.tz
Hati Miliki ©2017 Halmashauri ya Wilaya ya Ushetu . Haki zote zimehifadhiwa