USHETU KUANZA KUTEKELEZA MRADI WA REA NGAZI YA VITONGOJI 151.
Ushetu-kahama
Na. Emmanuel Shomary ,
07/05/2025.
Hayo yamebainishwa leo kupitia kikao cha robo ya 3 cha baraza la madiwani katika Halmashauri Ushetu wakati wa kupokea taarifa ya utekelezaji iliyotolewa na Meneja wa TANESCO kwa ngazi ya Wilaya ya Ushetu, Eng. George Madaha
Katika hatua Nyingine Eng. Madaha amesema, Ushetu kuna mradi mkubwa wa Umeme wa jua unaotekelezwa katika Kata ya Ukune kwenye Kijiji cha Kayenze, Umeme utakaozalisha Mega Wati 5 katika uimarishaji wa huduma.
Akizungumza kupitia kikao hicho, Diwani wa kata ya Nyankende, Mh Doah Limbu amemtaka Meneja Madaha kuisimamia kampuni ya NTONTAN kutoka China inayotekeleza mradi huo, ili iongeze kasi na umeme huo muhimu upatikane kwa haraka.
Kwa upande mwingine, Madiwani wa Ushetu, wamepongeza jitihada kubwa za Serikali katika kufanikisha mradi wa umeme ambao umeongeza ajira kwa Wananchi wa Ushetu kwa kufungua viwanda vidogo vidogo na pia matumizi ya kawaida.
Kwaupande wake Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo na ambaye pia ni Diwani wa Kata ya Igwamanoni, Mhe. Gagi Lala Gagi, amemuomba mkuu wa Wilaya ya Kahama, Mhe. Mboni Mohamed Mhita kushirikiana na vyombo vya Usalama ili kuendelea kuimarisha ulinzi na usalama kwenye Wilaya ya Kahama hasa kipindi hiki cha kuelekea uchaguzi mkuu.
Halmashauri ya Wilaya ya Ushetu
Anuani: S. L. P 50 Kahama
Simu: 0759888848
Simu ya kiganjani: 0759888848
Barua pepe: ded@ushetudc.go.tz Tovuti www.ushetudc.go.tz
Hati Miliki ©2017 Halmashauri ya Wilaya ya Ushetu . Haki zote zimehifadhiwa