Tume ya Maadili kwa watumishi wa Umma wafanya kikao na watumishi wa makao makuu Halmashauri ya Ushetu.
Na. Emmanuel Shomary,
Ushetu DC.
05 Mei, 2025.
KIKAO hicho chenye lengo la kuwakumbusha watumishi juu ya maadili ya Umma, kimefanyika leo katika eneo la wazi lililopo kwenye jengo la utawala la Halmashauri ya ushetu, na kuhudhuliwa na watumishi wote wa makao makuu.
Akiongea katika kikao hicho, afisa kutoka Tume ya maadili kwa watumishi Kanda ya Magharibi bwana
Fupala Mbwilo, amewataka watumishi wa Umma kuendelea kuwa waadilifu na wenye bidii katika kazi ili Wananchi waendelee lupata huduma bora.
'Watumishi wenzangu, Nimekuja ili tujikumbushe kuhusu maadili ya Utumishi wa Umma.
Tukumbuke kwamba, Serikali iliyopo madarakani imewekwa na Wananchi, hivyo Wananchi ndio Waajili wetu namba moja, hivyo ukimuona mwananchi anakuja ofisini kwako kupata huduma, basi fanya Kadri ya uwezo wako kuumpa huduma bora, maana huyo ndiye mwajili wetu" alisema Mbwilo.
Katika hatua nyingine, naye Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Ushetu, Bi. Hadija KABOJELA, amewataka watumishi hao kuendelea kuwa waadilifu na kufanya kazi kwa bidii ili lengo la kutoa huduma bora kwa wananchi liendelee kutimizwa.
"Sisi Ushetu, kwa asilimia 100, kazi zetu na hata huduma zetu zinagusa wananchi moja kwa moja, hivyo niendelee kuwakumbusha watumishi wenzangu, tuendelee kuboresha na kutoa huduma bora kwa wananchi, ili wananchi hawa waone fahari kwa kuhudumiwa na Serikali yao na hivyo wawe na upendo kwa Serikali yao". Alisema Kabojela.
Kikao hicho kilichoanza muda wa saa 3 na nusu asubuhi, kilitamatika saa 5 asubuhi, na wajumbe kupata kifungua kinywa kwa pamoja na Kisha kuendelea na majukumu yao ya kila siku.
Halmashauri ya Wilaya ya Ushetu
Anuani: S. L. P 50 Kahama
Simu: 0759888848
Simu ya kiganjani: 0759888848
Barua pepe: ded@ushetudc.go.tz Tovuti www.ushetudc.go.tz
Hati Miliki ©2017 Halmashauri ya Wilaya ya Ushetu . Haki zote zimehifadhiwa