Halmashauri ya wilaya ya Ushetu, imetoa kiasi cha fedha Tsh. 43,000,000/= ikiwa ni fedha ambazo zimekopeshwa kwa vikundi mbalimbali vya Wajasiliamali ili kuwawezesha kiuchumi. Jumla ya vikundi Kumi na Kimoja (11), ambavyo vimegawanyika katika makundi ya Vikundi vya Wanawake, Vikundi vya Vijana, na Kikundi cha Watu wenye Ulemavu Vimenufaika na uwezeshwaji huo.
Tukio hilo limefanyika leo tarehe 18 Oktoba, 2019, katika ukumbi wa Mikutano wa Halmashauri ya Wilaya ya Ushetu uliopo eneo la Nyamilangano.
Akizungumza wakati wa utoaji wa fedha hizo za mikopo kwa wajasiliamali, Mratibu wa Dawati la Uwezeshaji wananchi Kiuchumi, Bi. Minael John Ngomoi, amewataka wajasilimali hao kufanya kazi kwa Weledi mkubwa na kuwa na Ushrikiano wa dhati ili kuweza kufikia Malengo ya pamoja na kuweza kurejesha fedha hizo za mikopo kwa wakati.
Katika hatua nyingine, afisa biashara wa Halmashauri ya Ushetu, Bi. Beatrice Masesa, amewataka wana vikundi hao kuangalia fursa za biashara zilizopo katika maeneo yao ili wazitumie ipasavyo ili kupata tija kiuchumi katika shughuli zao.
Halmashauri ya Wilaya ya Ushetu
Anuani: S. L. P 50 Kahama
Simu: 0759888848
Simu ya kiganjani: 0759888848
Barua pepe: ded@ushetudc.go.tz Tovuti www.ushetudc.go.tz
Hati Miliki ©2017 Halmashauri ya Wilaya ya Ushetu . Haki zote zimehifadhiwa