• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua pepe |
    • Malalamiko |
Ushetu District Council
Ushetu District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Ushetu

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
      • Maadili ya msingi
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya msingi
    • Strategic Plan
  • Utawala
    • Idara
      • Elimu Sekondari
      • Elimu Msingi
      • Biashara na Fedha
      • Kilimo na Ushirika
      • Ujenzi
      • Maji
      • Afya
      • Usafi na Mazingira
      • Takwimu,Mipango na Uchumi
      • Maendeleo ya Jamii na Ustawi wa Jamii
      • Mifugo na Uvuvi
      • Land and Livestocks
    • Vitengo
      • Sheria
      • Manunuzi
      • Teknoloji Habari na Mawasiliano
      • Uchaguzi
      • Ufugaji Nyuki
      • Ukaguzi wa ndani
    • Muundo wa halmashauri
  • Fursa za uwekezaji
  • Huduma
    • Bima ya Afya
    • Mitambo ya kutengenezea Barabara
    • Loan Services
    • Huduma za Afya
    • Education Services
    • Water Services
    • Huduma za Kilimo
    • Livestock Keeping Services
    • Huduma za Uvuvi
    • Human Resources Services
    • Huduma za Leseni za Biashara
    • Land Services
    • Forest Services
  • Madiwani
  • Miradi
    • Uwekezaji
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Taarifa
    • Vifungu vya Sheria
    • Fomu za maombi
    • Zabuni
    • Miongozo
    • Hotuba
  • Kituo cha Habari
    • Hotuba
    • Uhifadhi wa picha
    • Video
    • Habari
    • Matukio

RC MACHA AFUNGUA MAONESHO YA NANENANE KANDA YA ZIWA MASHARIKI

Ilipo tumwa: August 4th, 2024

RC MACHA AFUNGUA MAONESHO YA NANENANE KANDA YA ZIWA MASHARIKI


Na. Emmanuel Shomary,

Ushetu DC


MKUU wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Anamringi Macha amefungua maonesho ya nanenane Kanda ya Ziwa Masharikii yanayofanyika viwanja vya Nyakabindi Bariadi mkoani Simiyu huku akiwataka Wananchi kutembelea maonesho haya ili wapate elimu, ushauri na maarifa mapya juu ya kuendesha kilimo na ufugaji wa kisasa kwani katika viwanja hivi kuna wataalam wengi mbalimbali kutoka mikoa ya Shinyanga, Simiyu, Mara na pia  Wizara zimeshiriki.


RC Macha ameyasema haya leo tarehe 3 Agosti, 2024 alipokuwa alipokuwa akihutubia mkutano mkubwa wa hadhara ambao umehudhuriwa na viongozi mbalimbali akiwemo Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Mhe. Kenan Kihongosi ambaye ndiye mwenyeji wa maonesho haya, alikuwepo pia Mkuu wa Mkoa wa Mara Mhe.Kanali Evans Mtambi, Makatibu Tawala wa Mikoa yote mitatu, Wakuu wa Wilaya, Wakuu wa Taasisi na wananchi ambao kimsingi ndiyo walengwa huku akipongeza kwa ujumla namna ambavyo maandalizi yamefanyika kufanikisha maonesho haya.


"Pamoja na pongezi kwa wandaaji wa maonesho haya, lakini niwaombe Wananchi wajitokeze kwa wingi hapa kwa siku hizi za maonesho ili wapate elimu, ushauri na utaalam kutoka kwa wabobezi wetu kuhusu namna bora ya kulima, kufuga na kufanya biashara kilimo, na uzuri wake ni kwamba vyote hivi vinafanyika bure bila gharama yoyote,"amesema RC Macha.


Awali akimkaribisha kuhutubia Wananchi, RC Kihongosi alisema kuwa uwepo wa maonesho haya Nyakabindi ni fursa kubwa sana kwa Wananchi wetu wa Mikoa hii mitatu ya Shinyanga, Mara na Simiyu kwani imekutanisha wataalam wa Serikali, Taasisi na Sekta binafsi


Maonesho haya ya nanenane yanatarajiwa kuhitimishwa ifikapo tarehe 8 Agosti, 2024 ikiwa ni kilele chake kwa Nchi zima huku yakitajwa kuwa na tija zaidi kwa Wananchi hususan wakulima ambao watapata fursa ya kukutana na wataalam, taasisi mbalimabali zikiwemo za kifedha na kilimo zenye kutoa elimu, mikopo ya vifaa vya kilimo na namna bora ya kufanya kilimo na ufugaji kuwa wenye tija zaidi kwa rasilimali chache.

Matangazo

  • Matokeo ya usajili wa Madereva. October 03, 2024
  • Tangazo la kuitwa kwenye Usaili August 22, 2022
  • Tangazo la kuitwa kwenye Usaili August 22, 2022
  • Tangazo la kuitwa kwenye Usaili August 22, 2022
  • Angalia yote

Habari mpya

  • RC MACHA AFANYA ZIARA YA KUKAGUA MAENDELEO YA MIRADI YA MWENGE HALMASHAURI YA WILAYA YA USHETU 2024/2025

    May 20, 2025
  • USHETU KUANZA KUTEKELEZA MRADI WA REA NGAZI YA VITONGOJI 151.

    May 08, 2025
  • Habari Picha: Watumishi wa Halmashauri ya Ushetu wakumbushwa kuhusu Maadili katika utumishi wa Umma

    May 07, 2025
  • Tume ya Maadili kwa watumishi wa Umma wafanya kikao na watumishi wa makao makuu Halmashauri ya Ushetu

    May 05, 2025
  • Angalia yote

Video

Kilimo cha Korosho katika Halmashauri ya Wilaya ya Ushetu
Video

Viunganishi vya haraka

  • Kanuni za Utumishi wa Umma
  • Ufafanuzi wa Serikali juu ya Kukosekana kwa Mawasiliano ya simu katika Halmashauri
  • Facebook
  • Ramani ya Halmashauri

Viunganishi Mfanano

  • Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma
  • Ofisi ya Rais-TAMISEMI
  • Baraza la Mitihani
  • Wizara ya Fedha
  • Wakala wa Serikali Mtandao
  • Ajira serikalini

World visitors tracker

world map hits counter

Idadi ya Waliotembelea

free HitCounter

Ramani ya Halmashauri

Wasiliana nasi

    Halmashauri ya Wilaya ya Ushetu

    Anuani: S. L. P 50 Kahama

    Simu: 0759888848

    Simu ya kiganjani: 0759888848

    Barua pepe: ded@ushetudc.go.tz Tovuti www.ushetudc.go.tz

Mawasiliano mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Hati Miliki ©2017 Halmashauri ya Wilaya ya Ushetu . Haki zote zimehifadhiwa