• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua pepe |
    • Malalamiko |
Ushetu District Council
Ushetu District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Ushetu

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
      • Maadili ya msingi
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya msingi
    • Strategic Plan
  • Utawala
    • Idara
      • Elimu Sekondari
      • Elimu Msingi
      • Biashara na Fedha
      • Kilimo na Ushirika
      • Ujenzi
      • Maji
      • Afya
      • Usafi na Mazingira
      • Takwimu,Mipango na Uchumi
      • Maendeleo ya Jamii na Ustawi wa Jamii
      • Mifugo na Uvuvi
      • Land and Livestocks
    • Vitengo
      • Sheria
      • Manunuzi
      • Teknoloji Habari na Mawasiliano
      • Uchaguzi
      • Ufugaji Nyuki
      • Ukaguzi wa ndani
    • Muundo wa halmashauri
  • Fursa za uwekezaji
  • Huduma
    • Bima ya Afya
    • Mitambo ya kutengenezea Barabara
    • Loan Services
    • Huduma za Afya
    • Education Services
    • Water Services
    • Huduma za Kilimo
    • Livestock Keeping Services
    • Huduma za Uvuvi
    • Human Resources Services
    • Huduma za Leseni za Biashara
    • Land Services
    • Forest Services
  • Madiwani
  • Miradi
    • Uwekezaji
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Taarifa
    • Vifungu vya Sheria
    • Fomu za maombi
    • Zabuni
    • Miongozo
    • Hotuba
  • Kituo cha Habari
    • Hotuba
    • Uhifadhi wa picha
    • Video
    • Habari
    • Matukio

“NINAWAAGIZA WAKURUGENZI NA WAKUU WA TAASISI ZOTE NDANI YA MKOA WA SHINYANGA KUWAPELEKA MAAFISA HABARI, MAWASILIANO NA UHUSIANO KATIKA MAFUNZO YA LUGHA YA ALAMA” - RC MACHA

Ilipo tumwa: September 26th, 2024


Na. Emmanuel Shomary, USHETU DC.

MKUU wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Anamringi Macha amewaagiza Wakurugenzi na Wakuu wa Taasisi zote Mkoani Shinyanga kuhakikisha kwamba Maafisa Habari, Mawasiliano, Itifaki na Uhusiano wanapelekwa kwenye mafunzo ya Lugha za alama ili waweze kusaidia mawasiliano katika utoaji wa huduma kwa Wananchi wakiwemo makundi maalum kama viziwi.

RC Macha ameyasema haya leo tarehe 25 Septemba, 2024 alipokuwa akifungua Maadhimisho ya  Wiki ya Viziwi Duniani ambayo yalianza tarehe 23 Septemba, 2024 na Kitaifa yanafanyika hapa mkoani Shinyanga ufunguzi ambao umehudhuriwa na viongozi mbalimbali wa Serikali, dini, Taasisi na watumishi ambao wamewezesha kuipamba shughuli hii huku akisisitiza kuwa lugha ya alama ni sawa na lugha nyingine duniani kama vile kichina nk.

"Nawaagiza Wakurugenzi wa Halmashauri na Taasisi zote ndani ya Mkoa huu kuhakikisha wanawapeleka mafunzoni Maafisa Habari, Mawasiliano, Itifaki na Uhusiano ili waweze kusaidia mawasiliano na utoaji wa huduma kwa wananchi na hasa makundi maalum wakiwemo viziwi kwani hawa ni wenzetu na wanazo haki zote kama binadamu wengine," amesema RC Macha.

Akimkaribisha Katibu Tawala Mkoa wa Shinyanga CP. Salum Hamduni  ili aseme neno, Mkuu wa Wilaya ya Kahama ambaye pia amekaimu Wilaya ya Shinyanga Mhe. Mboni Mhita amemshukuru sana Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kuwa mtetezi mkubwa wa watu wote wakiwemo viziwi, jambo ambalo linawapa nguvu wao wasaidizi wake kuendelea kutafsiri vema maono ya Mhe. Rais kwa vitendo hukumakiwakaribisha wageni wote wilayani Shinyanga na kwamba usalama upo wa kutosha sana na wananchi wake ni wakarimu sana.

Kwa upande wake RAS CP. Hamduni amesema kuwa maadhimisho haya yalinza tarehe 23 Septemba, 2024 na yatahitimishwa rasmi tarehe 28 Septemba, 2024 ambapo yanatarajiwa kufungwa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu - Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Ridhiwani Kikwete (MB). Kauli mbiu ya mwaka huu ni "Ungana Kutetea Haki za Lugha ya Alama".

Awali akitoa salamu za Chama cha Viziwi Tanzania Mwenyekiti Bi. Celina Mlemba amesema kuwa, maadhimisho haya ni utekelezaji wa Azimio la Umoja wa Mataifa la tarehe 9 Disemba, 1917 la kuzitaka nchi wanachama kufanya maadhimisho ya Wiki ya Viziwi Duniani kila ifikapo Septemba ya kila mwaka.

Matangazo

  • Matokeo ya usajili wa Madereva. October 03, 2024
  • Tangazo la kuitwa kwenye Usaili August 22, 2022
  • Tangazo la kuitwa kwenye Usaili August 22, 2022
  • Tangazo la kuitwa kwenye Usaili August 22, 2022
  • Angalia yote

Habari mpya

  • USHETU KUANZA KUTEKELEZA MRADI WA REA NGAZI YA VITONGOJI 151.

    May 08, 2025
  • Habari Picha: Watumishi wa Halmashauri ya Ushetu wakumbushwa kuhusu Maadili katika utumishi wa Umma

    May 07, 2025
  • Tume ya Maadili kwa watumishi wa Umma wafanya kikao na watumishi wa makao makuu Halmashauri ya Ushetu

    May 05, 2025
  • Tangazo la uuzaji Viwanja vya Makazi na Viwanda vidogo.

    April 16, 2025
  • Angalia yote

Video

Kilimo cha Korosho katika Halmashauri ya Wilaya ya Ushetu
Video

Viunganishi vya haraka

  • Kanuni za Utumishi wa Umma
  • Ufafanuzi wa Serikali juu ya Kukosekana kwa Mawasiliano ya simu katika Halmashauri
  • Facebook
  • Ramani ya Halmashauri

Viunganishi Mfanano

  • Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma
  • Ofisi ya Rais-TAMISEMI
  • Baraza la Mitihani
  • Wizara ya Fedha
  • Wakala wa Serikali Mtandao
  • Ajira serikalini

World visitors tracker

world map hits counter

Idadi ya Waliotembelea

free HitCounter

Ramani ya Halmashauri

Wasiliana nasi

    Halmashauri ya Wilaya ya Ushetu

    Anuani: S. L. P 50 Kahama

    Simu: 0759888848

    Simu ya kiganjani: 0759888848

    Barua pepe: ded@ushetudc.go.tz Tovuti www.ushetudc.go.tz

Mawasiliano mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Hati Miliki ©2017 Halmashauri ya Wilaya ya Ushetu . Haki zote zimehifadhiwa