Na. Emmanuel Shomary,
Ushetu DC.
Jul 02,2024.
Naibu Waziri wa Nishati Judith Kapinga, Amemuagiza Mkandarasi anayesambaza Umeme vijini (REA) Halmashauri ya Ushetu Wilayani Kahama Mkoani shinyanga Kuongeza kasi ya kusogeza huduma hiyo Kwa Wananchi.
Agizo hilo amelitoa leo 01 Julai,2024 katika mkutano wa hadhara uliofanyika Kijiji Cha Nsunga Kata ya Uyogo Baada ya kuwepo Kwa malalamiko yanayotokana na changamoto ya upatikanaji wa huduma hiyo Kwa wakazi wa eneo hilo.
"Nawaagiza makandarasi kukamilisha miradi kwenye maeneo yenu yote maana hakuna sababu ya kutokufanya hivyo, kwani Mhe. Rais ameshatoa fedha nyingi ili Wananchi hawa wafikishiwe Umeme" amesema Kapinga.
Katika hatua nyingine, Emmanuel Cherehani Mbunge wa Jimbo hilo amemuomba Mhe. Kapinga kupatikane gari maalumu kwaajiri ya kuwahudumia Wananchi wa Ushetu kulingana na ukubwa wa Jimbo hilo linalochukua asilimia 56 ya eneo lote la Wilaya ya Kahama.
"Mheshimiwa Naibu Waziri, Jimbo hili ni kubwa na linakata 20 na kifupi linachukuwa asilimia 56 ya eneo lote la Wilaya ya Kahama, mimi niombe mtupatie gari Ushetu kwaajiri ya kutoa huduma kwa Wananchi hawa, kutegenea magari ya wilaya ni changamoto" Alisema Cherehani.
Pia, baadhi ya Wananchi wa Ushetu wamelezea faida za Umeme namna ulivyowawezesha kuongeza ajira Kwa kuanzisha viwanda vidogo vidogo.
"Ukweli ni kwamba, kuja kwa umeme hasa kata ya Uyogo, kumesaidia sana kutoa ajira kwa Wananchi, mfano wa wazi ni pale makao makuu ya kata, pana Mashine kubwa ya kugredi mchele, ambapo vijana wamepata ajira, na akina mama ndio wamiliki hasa wa hicho kiwanda" Alisema Bahati Maige mkazi wa kijiji cha Nsuga kata ya Uyogo.
Halmashauri ya Wilaya ya Ushetu
Anuani: S. L. P 50 Kahama
Simu: 0759888848
Simu ya kiganjani: 0759888848
Barua pepe: ded@ushetudc.go.tz Tovuti www.ushetudc.go.tz
Hati Miliki ©2017 Halmashauri ya Wilaya ya Ushetu . Haki zote zimehifadhiwa