Naibu Waziri wa Mambo ya ndani Mh. Sagini Kirigini,(Mb) Ameahidi kuimarisha Ulinzi na usalama wa Wananchi Halmashauri ya Ushetu ikiwemo Ujenzi wa kituo kikubwa cha polisi na Ununuzi wa magari na Pikipiki za Doria Ili kuboresha utendaji kazi kwa askari katika kutimiza majukumu yao ya kila siku
Ameyabainisha hayo July 12 Mwaka huu katika mkutano wa hadhara ulifanyika kata ya Nyamilangano halimashauri ya Ushetu Wilayani kahama Mkoani Shinyanga kupitia ziara yake ya kukagua vituo vya polisi na kuzungumza na wananchi inayolenga kuimarisha usalama wa wananchi na Mali zao.
Hata hivyo Kiringini Amewataka wananchi kushirikiana na majeshi ya sungusungu kuhakikisha wanaimarisha suala la ulinzi wa wananchi kwakuwa askali pekee hawawezi kutatua changamoto hizo bila ushirikiano wa wananchi.
" Ndugu zangu niwaombe sana endeleeni kushirikiana na sungusungu Ili kuhakikisha maeneo yenu na Mali zenu zinakuwa salama jeshi la polisi linaaskari wachache ambayo hawawezi kuenea kikao sehemu wapeni ushirikiano wakutosha Ili tuweze kutokomeza uhalifu" Alisema Sagini.
Awali akizungumza kwenye mkutano huo Mbunge wa jumbo hilo Mh Emmanuel Cherehani Alielezea changamoto zinazowakabiri askari hao ikiwa nipamoja na ukubwa wa eneo la utawala na jiographia yake nakusisitiza wizara ifanye haraka katika kuwasaidia wananchi kwenye masuala ya ulinzi na usalama.
"Mh Naibi waziri kama nilivyokuomba tukiwa bungeni ufike jimboni kwangu ujionee hali ndiyo kama ulivyoona askari wako wanapata tabu sana kufika kwenye maeneo mengine jimbo nikubwa na kata ziko mbalimbali askari hawa hawana usafiri, na Hatuna jengo la kituo cha polisi na hapa tulipo Nyamilangano ndiyo makao makuu ya halimashauri nikuombe tu tena kupitia wizara yako mtusaidie KWA haraka Ili wananchi hawa wapiga kura wa Samia waweze kuishi KWA amani wakilindwa na polisi wetu" Alisema Cherehani.
Mkurugenzi mtendaji wa halimashauri hiyo bi Hadija Mohamed Kabojela Alisema Halmashauri iko salama wanaendelea kuhudumia Wananchi kama ilani ya chama cha mapinduzi inavyoekeleza.
Naye Diwani wa kata hiyo Mh Robert Mihayo Amesema kata iko salama na Wananchi wanaendelea na majukumu ya kikao siku ya kujitafutia kipato.
Mwisho.
Halmashauri ya Wilaya ya Ushetu
Anuani: S. L. P 50 Kahama
Simu: 0759888848
Simu ya kiganjani: 0759888848
Barua pepe: ded@ushetudc.go.tz Tovuti www.ushetudc.go.tz
Hati Miliki ©2017 Halmashauri ya Wilaya ya Ushetu . Haki zote zimehifadhiwa