Na. Emmanuel Shomary,
Ushetu DC.
MWENGE wa Uhuru umepokelewa na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Ushetu, Bi. Hadija Mohamed Kabojela, amekabidhiwa Mwenge huo na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Msalala, Ndugu Hamis Jafari katimba leo tarehe 14 Agosti, 2024 katika viwanja vya Shule ya Msingi Ukune kata ya Ukune, Pamoja na Mwenge huo wa Uhuru, Mkurugenzi wa Ushetu, pia amekabidhiwa wakimbiza Mwenge wa Uhuru sita (6), wakiongozwa na Ndg. Godfrey Mnzava.
Mwenge wa Uhuru ukiwa Halmashauri ya Ushetu, utakimbizwa kilometa 123 ili kuifikia miradi 8 yenye thamani ya Tzs. 2,384,866,193.82 kama ifuatavyo:
Mradi wa 1:
Mwenge wa Uhuru umezindua Vyumba vya madarasa 5, Shule ya Msingi Ukune kata ya Ukune, yaliyojengwa kwa thamani ya Fedha Tzs. 3,400,000, pamoja na maelekezo mengine kiongozi wa mbio za Mwenge Kitaifa ndg. Godfrey Mnzava amewataka Wananchi kutumia fursa hiyo ya Madarasa hayo ya kisasa zaidi ili kuwapeleka Watoto wao shule na kuwapa haki yao ya Msingi ya kupata Elimu.
Mradi wa 2:
Kuzindua Klabu ya Wapinga rushwa, shule ya Sekondari Kisuke.
Akizindua Klabu hiyo, Kiongozi wa Mbio za Mwenge Kitaifa, ameitaka jamii kuongeza nguvu na kujenga ushirikiano wa pamoja katika mapambano dhidi ya Rushwa, kwani Rushwa ni adui mkubwa wa haki.
Mradi wa 3:
Kuweka Jiwe la Msingi Mradi wa barabara Kilomita 1.05 kiwango cha lami Kata ya Nyamilangano. Mradi huo umegharimu kiasi cha fedha Tsz. 493,626,180
Pamoja na maelekezo mengine, Mkimbiza mwenge Kitaifa, amewahasa jamii kutumia Zaidi mfumo wa Manunuzi, NeST, ili kutoa zabuni kwa haki na kwa mzabuni aliyekidhi vigezo, ili kuepuka rushwa na ukosefu wa matumizi sahihi ya fedha za Serikali.
Mradi wa 4:
Kuwekwa jiwe la Msingi Mradi wa Ujenzi wa ofisi ya Machinga kata ya Nyamilangano. Ujenzi wa ofisi hii ya Machinga pamoja na bodaboda, Umegharimu fedha kiasi cha Tsz. 47,176,000.
Akiweka jiwe la Msingi katika mradi huo, Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa, amewapongeza Halmashauri ya Ushetu kwa mradi huo mzuri, kwani ni hatua nzuri katika kuwaletea maendeleo Wananchi hasa kundi kubwa la vijana.
Uwekaji wa jiwe la Msingi uliambatana na zoezi la kuteketeza madawa ya kulevya aina ya bangi kiasi cha kilogramu 34 lililotekelezwa na kiongozi huyo wa mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa.
Mradi wa 5:
Kuweka jiwe la msingi mradi wa Ujenzi wa bweni la wanafunzi wenye mahitaji maalum shule ya Msingi Nyamilangano, kata ya Nyamilangano.
Mradi huu umegharimu fedha kiasi cha Tsz. 135,567,000
Pamoja na maelekezo mengine, akiweka jiwe la msingi, Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru, amewapongeza Halmashauri ya Ushetu kwa Mradi huo, kwani Umethamini na kutambua wajibu wetu kama jamii, kuwahudumia na kuwaonesha upendo Watoto wenye mahitaji maalumu.
Zoezi la uwekaji jiwe la Msingi, umeambatana na ugawaji wa bidhaa muhimu kwa Watoto hao, ambapo Mafuta kwa ajili ya Watoto wenye Ulemavu wa Ngozi yamegawiwa Pamoja na Baiskeli 2 za matairi mawili (wheelchair).
Mradi wa 6:
Kukagua na kupanda miti (Upandaji miti) katika shule ya Sekondari Mapamba, Kata ya Mapamba.
Mradi huo wa Mazingira umegharimu kiasi cha fedha Tsz. 205,078,740
Katika Mradi huo, Ukaguzi ulifanyika na miti ikapandwa huku pia Wkimbiza mwenge wa Uhuru wakishiriki katika zoezi hilo. Akizungumza wakati wa zoezi hilo. Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuu Kitaifa, Amesisitiza umuhimu wa Viongozi wa Serikali kuchukua hatua za Kudumu katika utunzaji wa mazingira, badala ya kushiriki katika shughuli za upandaji miti wakati wa Mbio za Mwenge.
Mradi wa 7:
Kuweka jiwe la Msingi Ujenzi wa jengo la Tiba na Matunzo (CTC) Zahanati ya Mapamba, Kata ya Mapamba.
Mradi huu umegharimu fedha kiasi cha Tzs. 25,603,100. Akiwka jiwe la Msingi katika Mradi huo, kiongozi wa Mbio za Mwenge ameendelea kutoa maelekezo ya kukamilisha mradi mapema ili Wananchi wapate huduma hizo muhimu.
Mradi wa 8:
Kuweka jiwe la Msingi Ujenzi wa mradi wa Maji jijiji cha Chona kata ya Chona.
Mradi huu umegharimu fedha kiasi cha Tsz. 1,474,415,173.82.
Pamoja na maelekezo mengine, akiwekaja jiwe la Msingi, Kiongozi wa mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa, Amewataka Wananchi kutunza vema miundombinu hiyo ya maji ili iwafae wao sasa na hata kizazi kijacho.
Emmanuel Shomary Thomas,
AFISA HABARI HALMASHAURI YA USHETU.
Halmashauri ya Wilaya ya Ushetu
Anuani: S. L. P 50 Kahama
Simu: 0759888848
Simu ya kiganjani: 0759888848
Barua pepe: ded@ushetudc.go.tz Tovuti www.ushetudc.go.tz
Hati Miliki ©2017 Halmashauri ya Wilaya ya Ushetu . Haki zote zimehifadhiwa