MVUA KUBWA YALETA UHALIBIFU MKUBWA WA NYUMBA NA MAKAZI YA WATU KATIKA KIJIJI CHA BUTIBU KATA YA KINAMAPULA WILAYANI KAHAMA.
Butibu-Kinamapula, Ushetu.
Mvua zinazoendelea kunyesha sehemu mbalimbali Nchini, zimesababisha uhalibifu mkubwa wa nyumba na makazi ya watu katika kijiji cha Butibu kata ya Kinamapula wilayani Kahama.
Mvua hizo zilizoamabatana na upepo mkali, ngurumo na radi, zilianza kunyesha majira ya saa 10 alfajiri usiku wa kuamkia Jumanne Novemba 15, 2022, katika kijiji hicho, zilisababisha uhalibifu mkubwa ambapo jumla ya Majengo matatu (3) ya Taasisi na Majengo kumi na nne (14) ya watu binafsi yameharibika.
Majengo matatu ya Taasisi za Umma yaliyoharibiwa ni pamoja na:
Picha 1: Jengo la kanisa Katoriki Butibu lililoezuliwa paa.
Katika hatua nyingine, nyumba kumi na nne (14) za makazi ya watu binafsi zilizoharibiwa ni kama ifuatavyo:
Na.
|
Jina la mwenye Nyumba
|
Kitongoji
|
Madhara kwenye Nyumba
|
1
|
Hayati, Elias John Kwandikwa
|
Butibu A
|
Ukuta wa Fensi Umeanguka
|
2
|
Phabiani Stephano
|
Butibu A
|
Paa Limeezuliwa
|
3
|
Suzana Willium
|
Butibu A
|
Paa Limeezuliwa
|
4
|
Daudi Kanindo
|
Butibu A
|
Paa Limeezuliwa
|
5
|
Annastazia Martine
|
Butibu A
|
Paa Limeezuliwa
|
6
|
Joel Ernest
|
Butibu A
|
Paa Limeezuliwa
|
7
|
Mihangwa Lusupya
|
Shinyanga
|
Paa Limeezuliwa
|
8
|
Mateso Ramadhani
|
Shinyanga
|
Paa Limeezuliwa
|
9
|
Veronica Samsoni
|
Butibu B
|
Paa Limeezuliwa
|
10
|
Julius Kitobelo
|
Butibu B
|
Paa Limeezuliwa
|
11
|
Kulwa Kasala
|
Butibu B
|
Paa Limeezuliwa
|
12
|
Nyorobi Gamuga
|
Butibu B
|
Imeanguka
|
13
|
Charles Maziku
|
Nkuruungu A
|
Paa Limeezuliwa
|
14
|
Enos Majebele
|
Nkurungu A
|
Paa Limeezuliwa
|
Pamoja na uhalibifu huo, Mvua hizo pia zimesababisha wakazi watatu wa kijiji cha Butibu kudhulika ambapo bwana Julius Kitobeho aliangukiwa na tofali sehemu za kiunoni wakati akiwa katika harakati za kujiokoa na mvua hizo, ambapo hali yake inaendelea vyema bada ya kupatiwa matibabu katika zahanati ya Butibu kijijini hapo.
Kwa Upande mwingine, bwana na Bi Juma Ngulya nao walipata madhara ya kujeruhiwa na nyumba yao iliyobomolewa na mvua hizo, ambapo walipelekwa katika Hospitali ya Wilaya Kahama na hali zao zinaendelea vyema.
Picha 2: Jengo la darasa katika shule ya Msingi Butibu Lililobomolewa na Mvua hizo.
Akizungumza na wananchi wa kijiji cha Butibu, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Ushetu, Ndugu Linno P. Mwageni, amewapa pole Wananchi hao na pia kuwapa elimu ya namna ya kujikinga na madhara ya mvua, na katika hatua nyingine amewataka Wananchi hao kuwa watulivu katika kipindi hiki, ambapo Serikali inaandaa utaratibu wakuwasaidia Wananchi hao waliodhurika na Mvua hizo.
Picha 3: Nyumba ya ndg Julius Kitobelo iliyobomolewa na Mvua hizo.
Picha 4: Ukuta wa fensi ya nyumba ya hayati Elias Kwandikwa ulioanguka.
Halmashauri ya Wilaya ya Ushetu
Anuani: S. L. P 50 Kahama
Simu: 0759888848
Simu ya kiganjani: 0759888848
Barua pepe: ded@ushetudc.go.tz Tovuti www.ushetudc.go.tz
Hati Miliki ©2017 Halmashauri ya Wilaya ya Ushetu . Haki zote zimehifadhiwa