Na Ushetu DC, KAHAMA.
WANANCHI wa Halmashauri ya Ushetu Mkoani Shinyanga, wameondokana na adha ya kutembea umbali wa zaidi ya kilometa 100 kwenda na kurudi Hospitali ya Manispaa ya Kahama kupata matibabu, baada ya Serikali kununua vifaa vya wagonjwa wa dharuara katika Hospitali ya Halmashauri hiyo vyenye thamani ya TSh.milioni 500.
Mganga Mkuu wa Halmashauri ya Ushetu, Ndg. Athumani Matindo aliyabainisha haya wakati wa ziara ya Kamati ya Siasa ya Chama cha Mapinduzi (CCM) Mkoa ya kukagua Miradi mbalimbali ya Maendeleo.
Akiongea wakati wa ziara hiyo, Daktari Matindo alisema, awali walilazimika kusafirisha wagonjwa wa dharura mpaka Hospitali ya kahama ili kupata matibabu.
Dr. Matindo alivitaja baadhi ya vifaa hivyo kuwa ni pamoja na Digital X-ray, Ultrasound, Vitanda, Monitor pamoja na Ventilator vikiwa na thamani ya Sh.milioni 500 na kwamba mpaka sasa wameshatoa huduma kwa wagonjwa wa dharura 70 na amekuwa akihimiza kwa watoa huduma kuwa na lugha nzuri kwa wagonjwa.
Alisema, mwaka 2022 walipokea Sh.milioni 300 za kujenga kitengo cha Wagonjwa wa dharura, ambapo matibabu yake ilikuwa mpaka kusafiri umbali wa zaidi ya kilometa 100 kwenda na kurudi Hospitali ya Kahama,na wale wanaohitaji rufani ya kwenda Bugando wanatoka moja kwa moja, tofauti na awali walivyokuwa wanapita kwenye hospitali hiyo ya Kahama.
Mbunge wa jimbo la Ushetu, Mhe. Emmanuel Cherehani alisema, wapo baadhi ya Wagonjwa waliopo jirani na mikoa ya Geita na Tabora, walilazimika kwenda huko kupata matibabu, lakini baada ya kuwepo huduma ya wagonjwa wanje (OPD) na kitengo cha wagonjwa wa dharura Hospitali hiyo, hawajaenda tena Mikoa hiyo.
Pia Mh. Emmanuel alisema, amekuwa akipambana Bungeni kuhakikisha sekta ya Afya Halmashauri hiyo inaimalika na Wananchi wanapata huduma karibu na hivi karibuni wamepokea Sh.milioni 600 kati ya hizo Sh.300 zitatumika kununua vifaa tiba katika Zahanati ya Ulewe na Sh.300 pia kwenye kituo cha afya Igwamanoni.
Nae Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Shinyanga, Mhe. Mabala Mlolwa aliwapongeza kwa kuhakikisha Hospitali hiyo inakuwa na kitengo cha wagonjwa wa dharura.
Halmashauri ya Wilaya ya Ushetu
Anuani: S. L. P 50 Kahama
Simu: 0759888848
Simu ya kiganjani: 0759888848
Barua pepe: ded@ushetudc.go.tz Tovuti www.ushetudc.go.tz
Hati Miliki ©2017 Halmashauri ya Wilaya ya Ushetu . Haki zote zimehifadhiwa