"ILI KUPUNGUZA UTORO MASHULENI, TUNAPASWA KUANZISHA MASHAMBA YA CHAKULA KWA AJILI YA CHAKULA CHA WANAFUNZI"-Mhe DOA.
Na. Ushetu DC, KAHAMA
Halmashauri ya Ushetu Wilayani Kahama Mkoani Shinyanga, imetakiwa kuanzisha mashamba ya chakula kwa ajili ya chakula cha wanafunzi mashuleni ili kupunguza utoro pamoja na kuongeza ufaulu kutoka 80% kwa darasa la nne na 71% kwa darasa la saba na kuondokana na daraja D na E kwa wanafunzi.
Kauli hiyo imetolewa na mwenyekiti wa kamati ya Elimu, Afya na Maji Halimashauri ya Ushetu ambaye pia ni diwani wa kata ya Nyakende, mhe. Doa LIMBU katika kikao kazi cha tathimini ya mitihani ya shule za msingi, ambapo amesema kuna kila sababu ya kila shule katika Halmashauri hiyo kuanzisha mashamba ya shule kwa ajili ya chakula mashuleni ili kuongeza morari ya wanafunzi kufanya vizuri darasani.
Naye, Afisa Elimu Msingi wa Halmashauri ya Ushetu bi. Velena Ntulo, amesema kuhusu suala la chakula mashuleni, wazazi na walezi kupitia kamati za shule wanapaswa kushirikiana kwa pamoja na kuwajibika katika upatikaniji wa chakula mashuleni ili kutokomeza utoro mashuleni pamoja na kuongeza kiwango cha ufaulu.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Ushetu bi. Hadija KABOJELA, amewataka walimu wa shule hizo kushughulikia utoro kwa wanafunzi pamoja na kutokaa mbali na vituo vyao vya kazi ili kuendelea kuongeza ufaulu kutoka 80% hadi 100%.
Halmashauri ya Wilaya ya Ushetu
Anuani: S. L. P 50 Kahama
Simu: 0759888848
Simu ya kiganjani: 0759888848
Barua pepe: ded@ushetudc.go.tz Tovuti www.ushetudc.go.tz
Hati Miliki ©2017 Halmashauri ya Wilaya ya Ushetu . Haki zote zimehifadhiwa