Ofisi ya Rais-TAMISEMI kupitia fedha za IMF za kuimarisha huduma za Afya katika maeneo yaliyo athirika na UVIKO-19, imefanya ununuzi wa pikipiki 517 ikiwa ni sehemu ya uboreshaji wa huduma za afya kwa Wananchi.
Pikipiki hizo 517, zinatarajiwa kugawiwa kwa Halmashauri mbalimbali Nchini, ambapo miongoni mwa Halmashauri hizo zilizopata mgao huo wa pikipiki, Hakmashauri ya Wilaya ya Ushetu imepata pikipiki 3 aina ya BOXER 125 zenye namba za usajili STM 1923, STM 1924 na STM 1925.
Maafisa waliokabidhiwa pikipiki hizo kwa ajili ya kuratibu zoezi la kuboresha Afya kwa wananchi katika Halmashauri ya Ushetu ni
Akikabidhi pikipiki hizo leo tarehe 13 Oktoba, 2022, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Ushetu, ndg Linno P Mwageni, amewataka maafisa hao, kutumia vyombo hivyo vya Usafiri kwa makusudio yaliyokusudiwa ili kuleta tija na manufaa kwa Wananchi wa Ushetu.
Halmashauri ya Wilaya ya Ushetu
Anuani: S. L. P 50 Kahama
Simu: 0759888848
Simu ya kiganjani: 0759888848
Barua pepe: ded@ushetudc.go.tz Tovuti www.ushetudc.go.tz
Hati Miliki ©2017 Halmashauri ya Wilaya ya Ushetu . Haki zote zimehifadhiwa