HALMASHAURI YA USHETU YAGAWA PIKIPIKI 44, KWA MAAFISA UGANI 38 NA WATENDAJIWA KATA 6.
Pikipiki hizo zimegawiwa leo Machi 02, 2023 katika Ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Ushetu.
Akizungumza katika zoezi hilo la ugawaji wa pikpiki hizo aina ya Boxer 150, zilizotolewa na Serikali Kuu, Kaimu Mkurugenzi ndugu Deusi Anthony Kakulima, amewataka Maafisa Ugani Pamoja na Watendaji walipewa pikipiki hizo, kuzitumia vizuri ili kuleta tija kama Serikali ilivyo kusudia kuwahudumia Wananchi wake.
“Nawaagiza kuwa makini na pikipiki hizo, na mzitumie kwa ajili ya kuwahudumia Wananchi, hakikisheni mnafika kwa wakulima na kutoa huduma na ushauri wa kitaalamu, ili Wakulima wetu wa Ushetu tuone wakinufaika na Kilimo”, Alisema ndugu Kakulima.
Katika hatua nyingine, Mwenyekiti wa Halmashauri ya Ushetu, Mhe. Gagi Lala Gagi, amewataka maafisa Ugani hao Pamoja na Watendaji wa Kata, kuzitunza na kuzijali pikipiki hizo, ili malengo ya kuwahudumia Wananchi yatimie. “Ndugu zangu, naomba niwasihi sana, pikipiki hizo embu mzione kama ni pikipiki yako, uliyonunua kwa fedha zako mwenyewe, nawaomba mzitunze kwa uaminifu sana. Mjue Rais wetu Mama Samia anajali sana Wananchi wake, Angalia sasa alivyokuja na wazo la Kuwainua Wakulima kupitia ninyi, sasa hatutaki baada ya mwaka mmoja, Mama yetu Mpendwa Samia, aanze kuumiza kichwa tena kutafuta pesa kwa ajili ya pikipiki”. Alisema Mhe Gagi.
Nae mbuge wa Jimbo la Ushetu, Mhe. Emmanuel Cherehani, akiongea katika shughuli hiyo, amewataka Maafisa hao kuwa Wazalendo na wachapa kazi haswa, ili kilimo kiwe na tija kwa Wananchi wa Ushetu na Taifa kwa ujumla.
Halmashauri ya Wilaya ya Ushetu
Anuani: S. L. P 50 Kahama
Simu: 0759888848
Simu ya kiganjani: 0759888848
Barua pepe: ded@ushetudc.go.tz Tovuti www.ushetudc.go.tz
Hati Miliki ©2017 Halmashauri ya Wilaya ya Ushetu . Haki zote zimehifadhiwa