KATIKA kuifanya Ushetu kuwa ya kijani, kama yalivyo malengo na Makusudio ya Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo, Bi. Hadija KABOJELA, Halmashauri hiyo imeanza kuyaishi makusudio hayo kwa vitendo, kwa kuotesha miche ya Mikorosho na Mipapai na kuigawa kwa taasisi za Umma zikiwemo shule za Msingi na Sekondari na wakulima mbalimbali wa Halmashauri ya Ushetu
Akizungumza wakati wa zoezi hilo la ugawaji wa miche hiyo, Bi. Kabojela alisema " Ndugu zangu nawaomba sana muitunze miche hiyo, tumewapeni Mikorosho ambayo pia ni zao la biashara, na ni moja ya ubunifu tunaoufanya na CMT yangu kama chanzo kipya cha mapato na pengine kuwa mbadala wa Tumbaku, hivyo niwaombe muone kama ni fursa pia ya kujiinua kiuchumi, na niwaombe sana miche hiyo muipande kwa kufuata maelekezo ya kitaalamu ili ilete tija kwetu sote hapo baadae" alisema Kabojela.
Aliendelea pia kusema, " Lakini hata Mipapai hii, ni miche ya kisasa kabisa na inaanza kuweka matunda baada ya miezi sita tu, tena inaweka matunda kwa wingi sana, niwaombe tuone hii kama fursa kwetu" alimaliza Bi. Kabojela.
Katika hatua nyingine, bwana Emmanuel Gaga (fundi sanifu kilimo) na bwana Emmanuel Ngusa (Afisa Kilimo Mbogamboga, matunda na maua), ambao ndio wasimamizi na wazalishaji wa miche hiyo, wamemshukuru sana Mkurugenzi Bi. Kabojela kwa kufanikisha zoezi hilo ambalo pia ni endelevu kwa Halmashauri ya Ushetu.
Halmashauri ya Ushetu inajumla ya vitalu viwili, kimoja kipo Makao makuu ya Halmashauri Nyamilangano na kimezalisha jumla ya miche 10,500, ambapo Mikorosho ni miche 8,000 na mipapai 2,500.
Na Kitalu kingine kipo Kata ya Mpunze Chenye miche ya Mikorosho 8,000.
Halmashauri ya Wilaya ya Ushetu
Anuani: S. L. P 50 Kahama
Simu: 0759888848
Simu ya kiganjani: 0759888848
Barua pepe: ded@ushetudc.go.tz Tovuti www.ushetudc.go.tz
Hati Miliki ©2017 Halmashauri ya Wilaya ya Ushetu . Haki zote zimehifadhiwa