Ijumaa, 11 Julai, 2025.
Na Emmanuel Shomary
Ushetu DC.
Uzinduzi wa bodi ya Afya ya Wilaya, umefanyika rasmi leo tarehe 11 Julai, 2025, ikihudhuliwa na wajumbe wote akiwemo Mkurugenzi wa Halmashauri ya Ushetu, Bi. Hadija Kabojela pamoja na mgeni rasmi Bi. Glory Absalum ambaye ni kaimu Mkuu wa Wilaya ya Kahama.
Akitoa taarifa ya bodi ya Afya iliyomaliza muda wake, Katibu wa Afya Halmashauri ya Ushetu, bi Perpetua Ramadhani, amesema bodi iliyomaliza muda wake ilizinduliwa tarehe 22 Disemba 2021, ikiwa na jumla ya wajumbe 11 ambao wamehudumu kwa kipindi cha miaka 3 na kutimiza majukumu yao vema kwa mujibu wa muongozo.
Kwa upande mwingine, bodi hiyo mpya, imemchagua ndg Sadiki Paulo Tanganyika kuwa mweyekiti wake na pia bi. Nyanzige Joseph Gohebu kuwa Katibu wa bodi hiyo.
Akizungumza katika kikao hicho, Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya Ushetu, Bi hadja Kabojela, amewapongeza wajumbe hao wa bodi na kuwahasa kutumia nafasi waliyonayo kuwa sehemu ya uboreshaji wa huduma za Afya ndani ya Halmashauri ya Ushetu.
Katika hatua nyingine, mgeni rasmi Bi. Glory Absalum amewataka wajumbe hao kuwa sehemu ya utatuzi wa changamoto za huduma za afya, na sio kuuungana na Wananch kulalamikia huduma za afya, 'ndugu zangu, jamii imewapa dhamana ya kusimamia huduma za afya, hivyo tunategemea ninyi kuwa sehemu ya utatuzi wa changamoto za utoaji wa huduma hizo, na sio kuwa sehemu ya Wananchi wanaolalamikia huduma, Mwananchi akilalamikia huduma, kumbuka wewe ndio mtu wa kwanza kumsaidia' alisema Bi. Glory.
Kikao hicho kilitamatika majira ya saa 6 mchana na wajumbe walitakiana utekelezaji mwema wa majumu yaliyo mbele yao.
Halmashauri ya Wilaya ya Ushetu
Anuani: S. L. P 50 Kahama
Simu: 0759888848
Simu ya kiganjani: 0759888848
Barua pepe: ded@ushetudc.go.tz Tovuti www.ushetudc.go.tz
Hati Miliki ©2017 Halmashauri ya Wilaya ya Ushetu . Haki zote zimehifadhiwa