Na. Emmanuel Shomary.
Ushetu DC
MWENGE wa Uhuru umepokelewa na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Ushetu, Bi. Hadija Mohamed Kabojela, amekabidhiwa Mwenge huo na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Msalala, Ndugu Hamis Jafari katimba leo tarehe 14 Agosti, 2024 katika viwanja vya Shule ya Msingi Ukune kata ya Ukune, Pamoja na Mwenge huo wa Uhuru, Mkurugenzi wa Ushetu, pia amekabidhiwa wakimbiza Mwenge wa Uhuru sita (6), wakiongozwa na Ndg. Godfrey Mnzava.
Mwenge wa Uhuru ukiwa Halmashauri ya Ushetu, utakimbizwa kilometa 123 ili kuifikia miradi 8 yenye thamani ya Tzs. 2,384,866,193.82
Halmashauri ya Wilaya ya Ushetu
Anuani: S. L. P 50 Kahama
Simu: 0759888848
Simu ya kiganjani: 0759888848
Barua pepe: ded@ushetudc.go.tz Tovuti www.ushetudc.go.tz
Hati Miliki ©2017 Halmashauri ya Wilaya ya Ushetu . Haki zote zimehifadhiwa