Ushetu Kahama
Na Ushetu DC
01/02/2024
Kuelekea makadirio ya bajeti ya mwaka wa fedha 2024/2025 baraza la Madiwani Halmashauri ya Ushetu Wilayani Kahama Mkoani Shinyanga, limeidhinisha matumizi ya bajeti ya mwaka wa fedha 2023/2024 kupitia kikao barazahilo chenye agenda ya kuidhinisha makadirio ya budget mpya.
Awali akitoa taarifa kwenye baraza hilo, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri Bi. Khadija Kabojela amesema taarifa hiyo imepitia michakato yote kwa kuzingatia mapato na matumizi yam waka husika wa fedha.
"Mh Mwenyekiti na Baraza lote kwa ujumla, taarifa hii tumezingatia mapato na matumizi kwa kipindi chote mpaka leo tunaileta hapa kwenye kikao hicho cha baraza" Alisema Bi. Khadija
Akisoma taarifa ya matumizi ya bajeti hiyo Afisa Mipango wa Halmashauri ya Ushetu, Ndugu Shigela Kubeja Ganja amezitaja baadhi ya Idara ambazo Miradi ya maendeleo imetekelezwa.
"Halmashauri Kwa mwaka wa fedha 2023/2024 Miradi imetekelezwa kwenye sekta ya Afya, Kilimo, Elimu, Utawala na kulipa mishahala kwa watumishi" Alisema Ganja.
Katika hatua nyingine, Diwani wa kata ya Kinamapula, Mhe. Samweli Adriano amekishauri Kitengo cha fedha kuendelea kubuni njia za kuongeza mapato ya ndani ili kuchochea maendeleo zaidi.
"Mh Mwenyekiti mapitio ya bajeti yetu yako sawa, tunamuomba tu Mkurugenzi na Ofisi yake ya Fedha na Mipango waongezee bidii ya makusanyo ya ndani" Alisema Adriano.
Kikao hicho cha baraza kitaendelea tena siku ya pili kesho tarehe 02/02/2024, ikiwa ni mwendelezo wa baraza hilo la siku 2.
Halmashauri ya Wilaya ya Ushetu
Anuani: S. L. P 50 Kahama
Simu: 0759888848
Simu ya kiganjani: 0759888848
Barua pepe: ded@ushetudc.go.tz Tovuti www.ushetudc.go.tz
Hati Miliki ©2017 Halmashauri ya Wilaya ya Ushetu . Haki zote zimehifadhiwa