Na. Emmanuel Shomary,
Ushetu DC
Jumanne, 29 Julai, 2025.
MKUU wa Wilaya ya Kahama, Mhe. Frank Nkinda, amesema hayo leo terehe 29 Julai, 2025 kwenye kikao cha tathimini ya lishe, kilichofanyika kwenye ukumbi wa vikao uliopo Hospitali ya wilaya ya Ushetu na kuhudhuriwa na wajumbe mbalimbali akiwemo Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo Bi. Hadija Kabojela.
Akiongea katika kikao hicho, Mhe. Nkinda amewataka watendaji wa kata na wote wanaotekeleza afua za lishe, kushirikiana na wadau mbalimbali ili kuweza kufikia malengo kusudiwa.
"Swala la lishe sio la hiari, maana utekelezaji wake ni wa lazima, kwani haya ni maagizo ya Mhe. Rais, hivyo niwaombe mshirikiane na wanasiasa na wadau wengine, ili mnapokuwa huko vijijini kuwapa elimu Wananchi, inakuwa rahisi kama mkiwashirikisha wanasiasa na wadau wengine walio na ushawishi kwa jamii hiyo" amesema mhe. Nkinda.
Katika hatua nyingine, Mhe. Mkuu wa Wilaya, amewapongeza watendaji wa vijiji na Kata, kwa kazi nzuri wanazofanya katika kutekeleza afua za lishe na kuwataka waendelee kushirikishana uzoefu ili kwa pamoja wafikie malengo kusudiwa kwenye swala zima la lishe.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Halmashauri ya Ushetu, amewapongeza Divisheni ya Afya, Lishe na Ustawi wa Jamii pamoja na watendaji wa kata, kwa juhudi wanazofanya katika kutekeleza afua za lishe.
"Halmashauri imeendelea kufanya vema kwenye utekelezaji wa afua za lishe, lakini swala la Utapiamlo bado ni changamoto kidogohasa kwenye kuwabaini hawa watoto wenye utapiamlo,
basi Watendaji wa Kata na vijiji, fanyeni vikao kuanzia ngazi za chini kabisa, mkiwashirikisha Vitongoji, ili iwe rahisi kuwabaini hawa watoto wenye Utapiamlo na waanze matubabu mapema" amesema bi. Kabojela.
Kikao cha tathimini ya lishe, kinalenga kuimarisha maswala mazima ya lishe, ili kujenga uelewa mkubwa kwa jamii na kuwa na jamii yenye afya bora ya akili na mwili.
Halmashauri ya Wilaya ya Ushetu
Anuani: S. L. P 50 Kahama
Simu: 0759888848
Simu ya kiganjani: 0759888848
Barua pepe: ded@ushetudc.go.tz Tovuti www.ushetudc.go.tz
Hati Miliki ©2017 Halmashauri ya Wilaya ya Ushetu . Haki zote zimehifadhiwa